Home Education Muhtasari Wa Tumbo Lisiloshiba Na Hadithi Nyingine pdf

Muhtasari Wa Tumbo Lisiloshiba Na Hadithi Nyingine pdf

22

DownloadMwongozo Wa Tumbo Lisiloshiba Na Hadithi Nyingine(Pdf)

  • Muhtasari Wa Tumbo Lisiloshiba Na Hadithi Nyingine
  • Tumbo Lisiloshiba Na Hadithi Nyingine (Summary)
  • Tumbo Lisiloshiba Na Hadithi Nyingine (Pdf)
  • Mwongozo Wa Tumbo Lisiloshiba Notes
    Mwongozo Wa Tumbo Lisiloshiba Pdf
  • Uchambuzi Wa Hadithi Tumbo Lisiloshiba
  • Notes On Tumbo Lisiloshiba

Download pdf file

Mwongozo wa Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine

Wahariri

Alifa Chokocho na Dumu Kayanda (Longhorn Publishers) Waandishi

Maria Mvati

James Kanuri

Saul S. Bichwa

Dibaji

Mwongozo huu ni matokeo ya jitihada za Maria Mvati, James Kanuri na Saul S. Bichwa. The NES wameona kuwa ni muhimu kutayarisha mwongozo huu ili kuwasaidia walimu na wanafunzi katika kuelewa hadithi zilizosheheni humu.

Hata hivyo, inashauriwa kwamba msomaji wa mwongozo huu asome kwanza hadidhi zote kabla ya kupitia mwongozo huu. Kufanya hivyo kutatajirisha maarifa yanayopatikana katika mwongozo huu.

Mwongozo huu umetayarisha hadithi zote za Lisiloshiba na Hadithi Nyingine na kuzifanya zieleweke barabara. Kuna mifano ya maswali ili kuwapa changamoto watahiniwa wote.

Wanajopo waliotayarisha mwongozo huu wana tajiriba ya muda mrefu katika kufundisha somo

Ia Fasihi ya Kiswahili katika Shule za sekondari.

Ni matumaini yangu kuwa walimu na wanafunzi hawatachoka kuusoma mwongozo huu.

James M. Kanuri

Mkurugenzi

The National Educational Services 2017

Yaliyomo

1.1 Tumbo Lisiloshiba Said A. Mohamed 5

1.2 Mapenzi ya Kifaurongo Kenna Wasike -.15

1.3 Shogake Dadangu ana Ndevu Alifa Chokocho 26

1.4 Shibe Inatumaliza Salma Omar Hamad 34

1.5 Mame Bakari Mohammed K. Ghassany 41

1.6 Masharti ya Kisasa

1.7 Ndoto ya Mashaka

1.8 Kidege

1.9 Nizikeni Papa Hapa

1.10 Tulipokutana Tena

1.11 Mwalimu Mstaafu

1.12 Mtihani wa Maisha

1.13 Mkubwa

1.1 TUMBO LISILOSHIBA —Said A. Mohamed

Hadithi inaanza kwa taharuki kuhusu uvumi uliogeuka mnong’ono ukaeneza wasiwasi-hofu. Wasiwasi ulikuwa vibanda vitabomolewa vote. Watu wakubwa walitaka kuchukua makao ya watu ili kuendeleza ujenzi wao. Kwa Mzee Mago ndiko kituo cha kuzungumzia juu ya haki zao. Yeye huwakusanya wenzake iii wajadili juu ya haki zao za kuishi pale wanapochagua. Wanahojiana mambo juu ya:

➢  Kustahili kuishi kwa amani na furaha popote nchini mwao.

➢  Namna ya kuruka vikwazo vya sheria vilivyowekwa ili watu wadogo wasiweze kupoteza mali zao.

➢  Kushawishiana watafute wanasheria waaminifu iii kutatua (mazonge ya sheria).

Wanadai kuwa wanasheria waaminifu wameadimika —hakuna haki siku hizi.

➢  Kunasihiana na kuamshana juu ya kukubali maendeleo yanayopiga kasi nchini mwao.

➢  Maendeleo yanahitaji mchango wa kila mtu —mdogo kwa mkubwa, wa kike kwa wa kiume.

Mtu hawezi kukimbia ukweli, upya na usasa hutazamiwa kuleta mafanikio kwa watu wote. Mzee Mago huwaonya wauchunguze huo upya na usasa waujue jmst uhvyokaa —utaleta faida au hasara. Umaskini sio ujinga. Watu maskini wangeshauriwa wangeweza kuonyesha watakavyochangia maendeleo ya nchi yao. Watu wadogo hukasirika kwani wao hufanywa kuwa kama takataka. Hasira yao ndiyo inayowapa motisha wa kusema na kujitetea. Wakubwa walidai

kuwa jiji limejaa na halina nafasi tens, suluhisho ni kubomoa baadhi ya mitaa. Jiji limejaa hoteli, mikahawa, majumba ya Mall, maduka n k. Kwa hiyo, suluhisho la uhaba wa nafasi jijini ni kubomoa sehemu zingine. Mzee Mago aliwaleta wenzake pamoja kupigania haki za hapo Madongoporomoka —pasibomolewe.

Baadhi ya wanyonge hawa wanataka wapewe visenti vyao vichache vaondoke. Wengine wanadai, hakuna kuondoka. Wanataka vvabaki pale pale na kupigania haki zao. Kabwe alisisitiza kwa nguvu kuwa wakubwa hawataweza, kwani wanaogopa umma wa

Madongoporomoka. Bi. Suruta aliwatahadharisha kuwa wakubwa hawaogopi kitu chochote.

Wakati mjadala ukiendelea, chakula cha pale mgahawani kilikuwa tayari na kikaanza kunukia na kuwatamanisha wale waliobarizi hapo. Mara likatokea jitu kubwa na kukaa mle ndani. Jitu hilo liliamuru liletewe chakula Chote cha wateja wa Mzee Mugo. Jitu hilo lilifagia aina zote za vyakula: wali wa nazi, mchuzi, nyama ya kuchoma, kachumbari n k.

Baada ya kula vyakula vyote vya mgahawani hapo lililipa hela yote kisha likaahidi kuwa kesho tena lingekuja na liandaliwe chakula mara mbili ya kile kilicholiwa. Likawaacha kwa kitendawili kuwa, kesho kama wakiamka salama kama watafungua milango ya nyumba zao zilizosimama juu ya ardhi adhimu.

Alfajiri iliyofuata, polisi wakiwa na mirau na bunduki walikuwa wanalinda askari wa baraza la mji wakiviporomosha vibanda vyote.

Kulikuwa na mahangaiko ya wanyonge wasiwasi na hatan Mbio… Hawajui waokoe mali zao duni au nafsi zao kelele’ kwenzi vilio, malalamiko, vumbi (Uk 10).

Kumbe kile kitendawili cha jitu kilimaanisha kuwa ardhi Yao ingetwaliwa yote. Hata hivyo, wanyone wanashikilia msimamO wao kuwa fujo zisingeweza kuwaondoa katikia ardhi yao.

Baada ya wiki tatu za vurugu hilo; vibanda mshenzi Vya MadongoporomOka viliota, tena vingi kuliko vya awali.

ANWANI

  • Hadithi hii imepewa kichwa ambacho kinasadifu Yale yaliyomo. Wananchi wa

Madongoporomoka walisikia

uvumi kwamba kulikuwa na mpango wa kubomoa makao yao ili kutoa nafasi ya upanuzi wa jiji. Walijadiliana mara kwa mara wakiwa katika mkahawa mshenzi wa kiongozi wao Mzee Mago. Walijadili nini? Walitaka wapate suluhisho ili kujiauni na janga hilo, hawakuwa na makao mengine.

  • Wakiwa katika mgahawa huo wanaagiza vyakula mbalimbali. Linatokea jitu moja kubwa likatoa agizo kwamba lipewe vyakula vyote vilivyokuwa vimeandaliwa wateja wengine. Lilitishia kwamba wapende wasipende angejitwalia vyakula hivyo.
  • Jitu lilikula aina zote za vyakula na kunywa chupa kadhaa za soda. Mwishowe lililipa na kuahidi kwamba lingehitaji chakula mara mbili zaidi kesho yake. Siku iliyofuata, lile jitu litifika kuja ‘kula ardhi’ ya Madongoporomoka. Lile tumbo halishibi si chakula tu, bali rasilimali za raia kama ardhi.
  • Tumbo lisiloshiba husimamia wenye mamlaka ambao hawatosheki —wanamiliki mali nyingi lakini bado wanahitaji kumiliki kite kidogo walicho nacho wanyonge. Usasa na maendeleo yameleta ahueni kwa wananchi wachochole au yamezidisha unyanyasaji? DHAMIRA
  • Mwandishi amedhamiria kuonesha namna tabaka la juu linavyokandamiza haki za wanyonge. Tabaka hili linajilimbikizia mali na kutwaa rasilimali za wanyonge bila kushiba.

MAUDHUI

Ukatili na Dhuluma

  • Wakazi wa Madongoporomoka wanadhulumiwa ardhi yao. Tabaka la mabwanyenye wanawatoa katika ardhi you no kuwavunjia vibanda vyao pasipo hata kuwalipa fidia.

yao na kuwavunjia vibanda vyao pasipo hata fidia. Unyanyasaji huu unafanyika kwa kuwa wakazi

Madongoporomoka hawana mtetezi. Haki imenunuliwa wenye nacho. Hata hawajaoneshwa mahali mbadala watakwenda.

Matabaka

  • Hadithi hii inasawiri kuwapo kwa matabaka katika jamii. Kuna tabaka la mabwanyeye na tabaka la wanyonge. Tabaka la mabwanyenye linaendesha dhuluma dhidi ya wanyonge. Katika hadithi hii jitu kubwa linaonekam likisimamia shughuli ya ubomoaji wa vibanda vya wakazi wa Madongoporomoka. Tabaka hilo la mabwanyeye linatumia vyombo vya dola kama askari wa baraza Ia mji na askari polisi katika kuwakandamiza wanyonge.

Ukosefu wa Haki

Katika jamii iliyojaa dhuluma hakuna haki. Watu wa

Madongoporomoka wanaporwa haki yao ya kumiliki ardhi

Ardhi inatwaliwa na wenye nacho. Hata wanaposhauriana kutafuta wanasheria waaminifu bado wan ashindwa kuwapata. Wanasheria wamezibwa midomo kwa fedha za mabwanyenye. Haki

za watu zinasiginwa bila uteten wowote.

Umoja na mshikamano

  • Hata hivyo nguvu ya mnyonge ni Urnoja. Wakazi waMadongoporomoka wanaapa kuwa fujo hazitasaidia lolote. 1 yao kwa sababu ya fujo.

Baada ya wiki tatu za fujo hiyo wanaungana na kurejesha

WAHUSIKA

➢    Mpenda haki na mtetezi wa haki: yeye hakupuuza ule uvumi bali alijaribu kuutafutia

suluhisho

➢    Ni mwenye bidii: shughuli ya kupigania na kuzuia mipango ya watu wakubwa sio rahisi.

Ilibidi mzee Mago ajinyime, awatafute wenzake wazungumze na kulijadili jambo hili ambalo lilikuwa nyeti sana kwao.

➢    Ni mshawishi: aliwashawishi wanyonge wenzake watafute wanasheria waaminifu ili wasaidie kufafanua vipengele vigumu vya sheria kama njia ya kuwavukisha vikwazo ili wapate suluhisho.

➢    Ni mzindushi: aliwazindua wenzake na kuwapa nasaha kuhusu maendeleo. Aliwazindua kwamba maendeleo yanahitaji mchango wa kila mtu —wa kike kwa wa kiume, wadogo kwa waku bwa n k. Aidha, aliwatahadharisha kwamba wachunguze ni maendeleo gani yatakayowanufaisha.

Kabwe

➢  Anapenda ushirikiano. Alishirikianana wanyongewenzake katika kutafuta ufumbuzi wa kunyakuliwa kwa ardhi yao.

➢  Anaamini kuwa sheria inaweza kuwa suluhisho la matatizo yao.

➢  Ni mpenda amani na haki. Alitaka watafute suluhisho linalofaa kwa watu wa

Madongoporomoka.

Bi. Suruta

➢  Ni hodari katikakutoahojakwenye mashauriano. Anawapiku wanaume wote.

Bi. Fambo

➢  Mwanamke mojawapo wa wanyonge.

➢  Ni mwelewa masuala ya unyanyasaji.

➢  Anaeleza bayana kwamba wakubwa hawajali wanyonge wakihamishwa kwenye ardhi watakwenda wapi.

Jitu Ia miraba minne

➢  Hili lilikuwa ndovu —mtu kwa ukubwa wake.

➢  Ni mkubwa wa kimo: yeye alikuwa pandikizi la jitu Alipoingia katika mgahawa mshenzi watej a wote waligutuka

➢  Ni tajiri: mavazi yake ya suti na tai yalidhihirisha kuwa ni tajiri. Aidha yeye aliendeshwa na dereva wake maalum “chauffeur” katika gari Ia Audi Q 7.

➢  Ni mlafi: alikula vyakula vyote vya wateja waliokuwePO katika mgahawa wa Mzee Mago na kurudia mara tano kabl ya kushiba. Aidha alikunywa soda nyingi sana. vyakula vyote na hata hakusaza chochote.

Tanbihi; Ikumbukwe kwamba vyakula hivyo vilikuwa vimeagizva na wateja mbali mbali.

wote wamwachie vyakula vyao walivyokuwa wameagw a – wapende wasipende.

Anahusika katika uvamizi na unyakuzi wa ardhi ya

Madongoporomoka.

Umuhimu

  • Ni ishara ya wakubwa wa mji na sehemu nyingine ambao hawatosheki na mali nyingi walizo nazo. Daima hujinyakulia mali za wanyonge ili kuzidi kujinufaisha.

Maendeleo ni mazuri lakini wakati mwingine yanazusha mtafaruku katika jamii.

Wahusika wa makundi

Askari wa baraza la mji

➢  Hawa walibomoa vibanda vya wananchi wa  Madongoporomoka.

➢  Ni watiifu wa amri za wakubwa-hawakujali vilio na malalamiko ya wanyonge.

Kikosi cha polisi:

➢  Kinalinda askari wa baraza wakati wa kubomoa vibanda madongoporopoka.

Mbinu

Taharuki.

➢  Hadithi inapoanza kuna taharuki. Huo ni uvumi gani? Unazushwa na nani kwa sababu gani? Anaposema haukuwa wa kupasuka bomu au kulipuka mzinga anaendelea kuitilia uzito taharuki hiyo.

➢  Taharuki nyingine ni ile ya jitu liloingia mkahawa mshenzi lilitokea wapi? Kwa nini liliamua kuutembelea siku hiyo. Je ziara yake ni kula tu chakula au kufanya uchunguzi?

➢  Je jitu lenye tumbo kubwa lina uhusiano gani na kubomolewa kwa vibanda? Je ni kitu gani kilifanya vibanda vingi kushamiri baada ya kubomolewa?

Taswira

➢  Kuna taswira nyingi katika kisa hiki. Kuna taswira ya jitti la miraba mine kutokana na maelezo ya lile jitu lilivaa suti nyeusi na shati jeupe. Wakati mabuldoza yalipokuwa yakiangusha vibanda na kuwatimua watu. Ni taswira inayoangazia jinsi haki za

wanyonge zinavyofifishwa. Aidha jeshi la polisi hushadidia jambo hilo hilo la unyanyasaji wa w anyonge.

Balagha

➢  Haya ni maswali yasiyohitaji majibu, yanayomzindua mhusika.

➢  Mifano: yote hayo lakini yafae nini mbele ya nia ya kuhakikisha nafasi za biashara na malengo ya starehe ya wakubwa (Uk 10)

➢  Chupa mbili za Coca Cola zifae nini kwa jitu kuza kama hilo (Uk 8)

Mdokezo

➢  Maelezo machache ambayo hayakamiliki, yakitumiwa kuashiria jambo fulani. Lile jitu la miraba minne lilidokeza kwamba kungekuwa na tukio fulani. Kesho kama sote tutaamka salama. Kama tutafungua milango ya nyumba zetu zinazosimama juu ya ardhi hii adhimu.

Tashbihi

➢  Bweu lilipasuka kama mzinga (Uk 9)

➢  Kiti kilionekana kama cha Shule ya chekechea (uk 7)

➢  Kauli yajitu hilo ilimwinua Mzee Mago kama aliyechapwa bakora.

Kuchanganya ndimi

➢  Chauffeur (Uk ll)

➢  AudiQ7 (Uk10)

➢  Coca Cola

➢  Departmental stores, casinos (Uk 4)

Methali

  • Kuna matumizi ya methali kama kimya kingi kina mshindo

(Uk 3)

Takriri

➢  “Hawawezi, hawawezi kabisa hawawezi” (uk 5)

Mbinu rejeshi

➢  Uvumi kuhusu kubomolewa kwa vibanda ulianza halafu ukatoweka. Baadaye uvumi huo unarejelewa tena katika kibanda cha Mzee Mago.

Chuku

  • Ukubwa wa tumbo la mtu mwenye miraba mine limetiliwa.

chuku (uk 9)Kwa nini mwandishi amefanya hivi? Jim lilivyolamba sahani zote —halikubakisha hata ishara a chembe moja ya chakula chochote alichokula (Uk 9)

Taashira

➢  Msitari wa fedha ulipasuka kutoka mbinguni hii ni ishara za matumaini, mwangaza au nuru huashiria jambo jema.

➢  Hali ya mstari huo kumulika mpaka ndani ya mioyo ya watu na wakati huo huo uso wa lile jitu lisiloshiba kuonekana

Hii ishara ina maana kuwa ndani ya nafsi za wanyonge wakiongozwa na Mzee Mago wanajua kuwa taabu zao zinatokana na wale wakubwa wasioshiba —wakiwakiJishwa najitu ndani ya Audi Q 7.

MAPENZI YA KIFAURONGO —Kena Wasike

Muhtasari

Kifauongo ni mmea ambao majani yake hujikunyata yanapoguswa.

Dennis ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu ch Kivukoni. Ndani ya nafsi yake anasononeka kwa ufukara uliomwandama yeye na familia yak-e. Umaskini unamsumbua maana hali yake na ya watoto wa matajiri ilikuwa zimeachana wazi kabisa kama mbingu na ardhi.

Kulikuwa na tofauti katika mavazi, chakula, simu na vifaa vingine kisasa. Hali ya umaskini inamfanya asielewe yale ambayo mhadhiri

Dkt Mabonga alikuwa akiwafundisha. Licha ya tatizo lake la umaskini, Dennis amekabiliwa na ugumu wa somo hili. Dkt

Mabonga aliwakatisha tamaa wanafunzi wake kutokana na shutma zake kwamba wao hawafikirii na kutafakari mambo kwa kina kama wanafunzi wapevu wa Chuo kikuu. Alipoulizwa maswali aliwakashifu kwamba hawastahili kuwa humo kwenye darasa Ia chuoni.

Kwa Dennis hili liliongeza uzani zaidi wa tatizo lake. Dennis hakuweza kuchangamana na wanachuo wakwasi. Kulikuwa na matabaka —wenye jadi kubeli wanapitajuu na wachochole wanapita chini (Uk 17). Wanafunzi wakwasi walipoona masomo yanatatiza walikuwa na fursa ya kurejea makwao na kuendeleza miradi ya wazazi wao. Kwa Dennis hili lisingewezekana. Wazazi wake walikuwa wanategemea vibarua vya kulima mashamba ya watu

Wengine. Yeye ndoto yake ilikuwa kumaliza masomo na kupata kazi ili aweze kuumaliza ukata wake na wazazi wake.

Umaskini wake ulimfanya asiwazie hata kuwa na rafiki wa kike. Penina msichana wa tabaka Ia juu anamtembelea Dennis na kutaka

Wawe marafiki. Dennis analipinga jambo hilo kutokana na tofauti zao za kitabaka; lakini Penina anang’ang’ania kuwa tofauti zao kiuchumi haziwezi kuwa kikwazo. Penina alitaka mwanaume

ambaye ni mwaminifu. Anasisitiza, “Nataka tupige vita fikra kwanlba kijana wa kitajiri hawezi kutangamana na mwenziwe

(Uk 21)

Mapenzi ya Penina aliyetoka katika familia ya wakwasi na Dennis tkara yalidumu kwa miaka miwili. Baada ya kumaliza Chuo walnshi mtaa wa watu wastani kimapato. Pamoja najitihada zoteza kutatilta kazi. Dennis hakufanikiwa. Barua zake nyingi alizotuma hazikumletea tumaini lolote.

Fursa moja aliyopata katika shirika Ia uchapishaji magazeti aliipoteza baada ya kushindwa kujibu swali la kwanza katika mahojiano.

Mapenzi ya kifaungo ya Penina yanajitokeza wazi. Anamfukun

Dennis na kumwonya kwamba nyumba yake aione paa. Alielezea majuto yake ya kusuhubiana naye na kumkanya kwamba asije akaelezea watu wengine kwamba waliwahi kupendana.

Dennis alifungasha nguo zake na kuondoka akiwa haamini. Kumbe mapenzi ya Penina yalikuwa ya kifaurongo.

ANWANI

  • Anwani ya hadithi hii ni “Mapenzi ya Kifaurongo.Kifaurongo ni mmea ambao unajikunja Pindi tu unapuguswa na hujikunjua baada ya muda mfupi. Katika hadithi hii mhusika Penina anampenda Dennis kwa kuwa alikuwa mwaminifu. Walimaliza masomo yao lakini baada ya miaka miwili, kutokana na ukosefu wa kazi mapenzi yake yalididimia na kunyauka kabisa. Hakutaka kuhusishwa tena na Dennis. Alimfukuza kama mbwa. Ahadi zake za mapenn

zikawa kama za ule mmea. Dennis alihitaji kazi na alikuwa na ari ya kufaulu usaili lakini; anaulizwa swali moja tu na ananywea na kushindwa kujibu na hivyo anarudi nyumam bila tumaini lolote.

huduma ni sawa na mmea wa kifaurongo. Anaonesha Kuwa penzi la Penina na Dennis linanyauka baada ya Dennis kukosa kazi ambayo ingcmpatia kipato cha kumhudumia mkewe.

MAUDHUI

Ndoto za maisha.

➢  Wazazi wa Dennis walifanya juu chini ili waepukane na ukata lakini uliendelea kuwaandama. Walimsomesha Dennis wakitegemea kwamba baadaye angewasaidia lakini Dennis hakufanikiwa kupata kazi. Dennis alikuwa na ndoto zake. Alitaka kufaulu vizuri-hii ndoto ilitimia. Alitarajia kupata kazi baada ya kuhitimu ndoto hii haikutimia, licha ya yeye kuandika tawasifu yake na kuituma sehcmu nyingi.

➢  Aidha, Dennis alikuwa na matarajio ya kumwoa mchumba wake Penina. Hilo halikutokea, na isitoshe waliachana kwa njia mbaya-Penina alimfukuza atoke kwake.

➢  Dennis alikuwa na ndoto ya kuwa mtangazaji wa redio. Alifanya mazoezi mengi na kujipatia ujuzi ambao watu wengi waliafiki kwamba atakuwa mtangazaji bora mno. Hata hivyo ndoto yake hiyo haikutimia.

Matabaka

  • Dennis anatoka katika familia maskini. Wazazi wake walikuwa wachochole, hawakuwa na mali yoyote. Waliiitahidi sana kutoka katika ufukwe huo haikuwezekana walimiliki majumba mengi na wengine walikuwa misururu ya mabasi na matatu ya abiria. Shakila alikuv wa tabaka la juu —mama yake alikuwa mkurugenzi tnku wa shirika la uchapishaji. Wanachuo waliotoka tabaka laju walikuwa na maisha mazuri, libasi (nguo) zao ni bora, wan; simu nzuri, tarakilishi na vitu vingine. Dennis mavazi yak, valikuwa duni, kula kwa shida na kadhalika.
  • Kulikuwa na watu walioendesha magari ya kifahari makubwa na mazuri. Wazazi wa Dennis ni wa tabaka la chini. Walifahamu kuweka majembe begani na kulima vibarua tu.

Umuhimu wa kazi.

  • Kilabinadamu lazima afanye kazi. Kazi humzatiti binadamu. Elimu hutumiwa kama kidato cha kujipatia kazi. Kazi ndiyo msingi wa maisha. Maisha hayawezi kusonga mbele kama hufanyi kazi yoyote. Kitendo cha Dennis kukosa kazi, kinamfanya aonekane kama mzigo asiye na faida yoyote kwa Penina. Penina anaamua kuachana naye na kumfukuza kabisa atoke kwake

Mapenzi

  • Wanafunzi wa Chuo cha Kivukoni wanaonekana wengi wao kuwa na mahusiano ya kimapenzi. Wale wa tabaka muia huonekana wakiongozana mvulana na msichana kufanya starehe za hapa na pale.
  • Aidha, Penina mtoto kutoka katika tabaka la wenye nacho, anasalitiwa na mpenzi wake ambaye naye ni wa tabaka la juu. Katika kutafuta suluhisho Ia mapenzi ya dhati Penina anaamua kupelcka mapenzi yake kwa Dennis ambaye anatoka katika tabaka la chini. Mapenzi yao yananoga kama kinu na mchi wakati wakiwa chasm. Penzi linakuja kuwa Ia kifaurongo pale wanapomaliza chuo na Dennis kukosa kazi

Wahusika

Dennis

➢  Kutokana na ukata wa wazazi wake, Dennis anaishi maisha ya kimaskini chuoni.

➢  Anakuwa mpweke chuoni. Umaskini wake ulimfanya asijiamini na aghalabu alikuwa mwenye huzuni. Anaisitikia hali yake duni, akawa msononevu.

➢   Anabahatika kupendwa na Penina, msichana mrembo kutoka familia ya kitajiri. Mvuto wa Penina unamfanya Dennis abadili msimamo wake wa awali-akasalitika na kukubali kuwa na mahusiano naye.

➢  Ukosefu wa ajira unamfanya afukuzwe na Penina-akajikuta mpweke tena asiye na makao. Kauli ya Dennis ya hapo awali ikatimia; “Mapenzi hukua, huugua yapatapo maradhi na hufa” (Uk 20)

➢  Ni mvumilivu: anavumilia hali yao ya umasikini na ukosefu wa vifaa vya kisasa alipokuwa chuoni.

➢  Ana bidii: anajitahidi sana katika masomo hadi akafaulu vyema. Alisomea kijijini kwenye shule za kawaida lakini akafaulu na kuingia chuo kikuu.

➢  Alitafuta kazi kwa bidii, alituma tawasifu yake mahali pengi.

➢   Ana tamaa: alitamani awe na rafikimpenzi kama wanachuo wengine. Kuwa na gari la kifahari-“Sikomi kuyamezea mate hayo”. Alitamani hali njema ya siha mavazi bora ya watu wakwasi. Alitamani wazazi wake wangekuwa matajiri

Kutokana na ukata wa wazazi wake, Dennis anaishi maisha ya kimaskini chuoni. Anakuwa mpweke chuoni. Umaskini wake ulimfanya asijiamini na aghalabu alikuwa mwenye huzuni. Anaisitikia hali yake duni, akawa msononevu. Anabahatika kupendwa na Penina, msichana mrembo kutoka familia ya kitajiri. Mvuto wa Penina unamfanya Dennis abadili msimamo wake wa awali-akasalitika na kukubali kuwa na mahusiano naye. Ukosefu wa ajira unamfanya afukuzwe na Penina-akajikuta mpweke tena asiye na makao. Kauli ya Dennis ya hapo awali ikatimia; “Mapenzi hukua, huugua yapatapo maradhi na hufa” (Uk 20)

Ni mvumilivu: anavumilia hali yao ya umasikini na ukosefu wa vifaa vya kisasa alipokuwa chuoni. Ana bidii: anajitahidi sana katika masomo hadi akafaulu vyema. Alisomea kijijini kwenye shule

za kawaida lakini akafaulu na kuingia chuo kikuu.

Alitafuta kazi kwa bidii, alituma tawasifu yake mahali pengi. Ana tamaa: alitamani awe na rafikimpenzi kama wanachuo wengine. Kuwa na gari la kifahari-“Sikomi kuyamezea mate hayo”. Alitamani hali njema ya siha mavazi bora ya watu wakwasi. Alitamani wazazi wake wangekuwa matajiri

Mwenye hasira: anamkashifu Dennis kwa kasbfa no kukosa kazi,

Umuhimu Wake

Ametumiwa kuangazia ugumu wa kupata apra hata ya kupata shahada. Aidha. Dennis ametumika kudhihirisha kuwa si Rihisi kijana wa kiume mchochole kupendwa na msichana wa tabaka la juu na mahusiano yao kudumu.

Penina

  • Mwanachuo wa Chuo kikuu cha Kivukoni.
  • Msichana kutoka kwenye familia yenye utajiri mwingi.
  • Baba yake Bw. Kitime ni Katibu wa kudumu katika Wizara ya Fedha.
  • Penina anapata masurufu mengi ya kutosha, shilingi elfu tano kila juma.
  • Ni mshawishi: alimshawishi Dennis kuwa pesa na mapenn ni vitu tofauti. Dennis alikubaliana naye.
  • Ana tamaa ya mapenzi: ingawa alipewa pesa za kutosha alikuwa na majonzi kwa ajili ya kukosa mpenzi.
  • Ni jasiri: alimpasulia Dennis ukweli kuwa amempenda na anataka wawe wapenzi badala ya kusubiri afuatwe yeye.
  • Hana uvumilivu sana: aliweza kukaa na Dennis kwa miaka miwili tu akamtupa nje ya nyumba yake.
  • Ni mwenye msimamo: alikata kauli ya kupendana na mwanaume asiye na pesa. Alitoa uamuzi kwamba hataolewa mpaka Dennis apate kazi kubwa. Alipokosa ajira anamfukuza na kumtukana.
  • Hana subira: aliweza kumvumilia Dennis kwa kipindi Cha miaka miwili tu-
  • Mwenye hasira: anamkashia Dennis kwa kashfa kali kutokana na kukosa kazi.
  • Mdadisi: aliweza kujua jina Ia Dennis hadi chumba chake katika Mastura Hall. Alijua kuwa Dennis hana fedha na kumweleza bayana.

Umuhimu

Anadhihirisha kuwa sio rahisi msichana wa tabaka Ia juu kuolewa na mvulana mchochole.

Dkt Mabonga

  • Mhadhiri wa Chuo kikuu.
  • Anaifahamu mada yake ya fasihi vyema.
  • Anakatisha wanafunzi tamaa kwa majibu yake ya mkato na makavu.
  • Mkweli: hasiti kusema yale yaliyomo moyoni hata kama yataleta maudhi.
  • Ingawaje ni msomi anashindwa kuwafafanulia wanafunzi wake dhana ngumu zinazowatatiza.

Umuhimu

  • Ametumiwa kudhihirisha ugumu wa masomo ya Chuo kikuu na namna walimu wanavyohitaji wanafunzi watafute maarifa wao wenyewe.

Shakila

  • Mwanachuo na mwanamji wa Kivukoni.
  • Msichana am baye hakupata shida za kutafuta kazi.
  • Ana mlahaka mwema: anamkumbuka na kumsalimia vizuri Dennis wakati Dennis ameenda kuomba kazi.
  • Ni mwenye maiivuno
  • Ni mwenye majivuno: alijigamba chuoni kwamba yake ni mkurugenzi wa shirika moja la kuchapisha
  • Ni mfariji: anampa moyo Dennis kwamba Mungu apate kazi ile.

Umuhimu

  • Kudhihirisha matabaka yaliyo katika jamii.

Bwana na Bi. Kitime

  • Hawa ni wazazi wa Penina.
  • Bwana Kitime ni Katibu wa kudumu wa Wizara ya Fedha.
  • Ni wakwasi, wako katika daraja la juu.
  • Wanamtumia binti yao fedha za kutosha kila wiki.
  • Wanampa binti yao malezi ya hali yajuu kwani wanajiweza.
  • Wanawapatia Penina na Dennis masurufu yote wakielewa fika kuwa hawana kazi.
  • Ni washauri: walimtahadharisha Penina kuhusu kuolewa na mchochole asiye na kazi.

Hata hivyo walimwachia Penina uhuru wa kujiamulia.

Mbinu

Taharuki

  • Kuna taharuki, wakati mlango wa Dennis unapogongwa: Mja huyo ni nani, Penina alijuaje kuwa huyu kijana anaitwaDennis.
  • Wakati kisa kinapomalizikia pia kuna taharuki: Je Dennis alienda wapi? Alipata mastakimu vipi bila fedha? Penina aliendelea kuishi katika nyumba ile.

Balagha

  • Wavulana wangapi wamejikuta wakining’inia bila kupenda kwao’? (Uk 18)
  • Kwani swali langu liko vipi? Kwa nini wanafunzi anacheka? Maswali haya yanamhusu

Dennis. Kwa nini ninalia sasa (Uk 13)

  • Fukara aliyefukarika mpaka mwisho aseme mm mbele ya wanaojigamba na kujishaua?(Uk 16) …
  • Nitawalipaje wazazi wangu wema walionitendea (Uk 25)

Tashbihi

  • Ninahangaika kama kondoo aliyevamiwa na jeshi la usubi (Uk 25)
  • Nimetoka ofisini kama mgonjwa mahututi.
  • Nimeweweseka kama ubua (Uk 25)
  • Mapenzi ni matamu kama uki (Uk 16) Yametengana kama ardhi na mbingu (Uk 17)
  • Njaa inanitafuna kama mbwa anavyouguguna mfupa (Uk 17)
  • Kutetemeka kama aliyenyeshewa na mvua kubwa kumwibua bingwa ni kama kupata maziwa kutoka kwa kuku (Uk 13)

Methali

  • Mzoea sahani vya kigae haviwezi (Uk 20)
  • Ujapokosa la mama hata la mbwa huanwa (Uk 17)
  • Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura (Uk. I 5)
  • Mtu huvuna alichopanda (Uk 20)
  • Mzungu wa kula haufunzwi mwana (uk 15 )
  • Mgomba changaraweni haupandwi ukamea (Uk 27)

Misemo

  • Hazipunguzi hazizidishi (uk 21)

Utabiri

  • Dennis alitabiri vile ambavyo Penina alimpenda wakati huo” akasema kesho anaweza kuwa chanzo cha kero na usumbufu. Huba litakuwa limekufa na kufukiwa kaburini.
  • Hili lilitokea baada ya kukaa kwa miaka miwili na mchumbake Penina.

Litifai

Kuna maneno yaliyodondolewa katika riwaya ya utengano “Na nyumba hii uone ” (Uk 27)

Kuchanganya ndimi

  • Your competence is doubtful, (uk 25)
  • Tarmacking (uk 26)

Mjadala wa nafsi

  • Dennis anapofukuzwa anajizungumzia sijui kama mimi ndiye kupe au mlazadamu.

1.3 SHOGAKE DADA ANA NDEVU —Alifa Chokocho

Bwana Masudi na Bi. Hamida ni mtu na mkewe. Wamejaliwa kupat binti aitwaye Safia. Kabla ya kulala wazazi hawa huzungumz mambo mazito yanayogusa mioyo yao. Walimsifia sana binti

yao kwa vile alivyo na mwenendo mzuri. Safia ana tabia inayowafurahisha wazazi wake. Shuleni anafanya vyema kabisa. Wazazi hawa walielewa vyema kabisa kuwa kupata mtoto na kumlea ni mambo mawili tofauti “…kuzaa mwana si pato, pato ni kumvyeleza “

(Uk 29)

Walijadili ukweli kwamba wapo wazazi waliojali wa watoto, lakini wakawa balaa. Wakakosa manufaa kwa wazee wao na jamii nzima.

Bi. Hamida anatoa mfano wa mtoto wa Habiba Chechei aitwaye Mkadi. Mkadi ana vitendo viovu kushinda shetani. Walimlinganisha Mkadi na Safia na kuona binti yao ni safi hana doa.

Sifa nzuri za Safia zilienea hadi kwa marafiki na watu wote wanaoingia na kutoka kwa Bwana na

Bi. Masudi. Kwa nini anasifiwa hivyo?

  • Husaidia wazazi wake.
  • Husaidia kazi zozote habagui.
  • Yeye ni hodari sana shuleni.
  • Kila mtihani huibuka wa kwanza.
  • Humwogopa Mungu na kufuata sheria zake zote.
  • Safia hujiongoza na kufanya hayo yote bila kushurutishwa na mtu yeyote. Hayo yote aliyalifanya wazazi wake wakashukuru kupita kiasi.

Safia aliwataka wazazi wake wamruhusu Kimwana shoga yake aje ili wajitayarishe vyema kwa mtihani wa kuingia kidato cha kwanza.

Wazazi wa Safia walikubali wasemavyo wahenga kuwa, . kidole kimoja hakivunji chawa. Analolijua Safia, Kimwana halijui.

analolitambua Kimwana Safia hana habari nalo e ” (Uk 31)

Wk 30 Baada ya muda, Kimwana akaanza kuja nyumbani kwa akina Safia na wakawa wanasomea chumbani. Wakaomba kufunga mlango ili wasisumbuliwe na Lulua, ndugu mdogo wa Safia. Wazazi wao wakawaruhusu wafunge mlango kwa ndani. Baada ya muda kupita, Bi. Hamida akawa ana shaka ya kuwa Safia ni mjamzito. Akaanza kuona dalili zote —kutapika na kunyong’onyea na hana uchangamfu. Alipomdadisi, Safia alikasirika na kumlaumu mama yake. Hata hivyo Bi. Hamida alitia shaka, akachanganyikiwa-Safia anasema uongo au ukweli. Alimuuliza mumewe, ambaye alisema kuwa Safia hawezi kuwa mjamzito. Siku moja wakila chamcha, Lulua alitoboa siri kwamba, aliingia chumbani mwa Safia akawakuta wamelala. Na shogake Safia alimwona ana ndevu. Wakati huo huo Bw. Masudi akapata ujumbe kwa simu uliomgutusha —Safia aliyekwenda kliniki kutoa mimba amekufa. Bi. Hamida na Bw. Masudi wakachukue maiti.

ANWANI

➢  Anwani ya hadithi hii inasadifu yale yaliyomo. Safia binti wa Bwana Masudi na Bi.

Hamida anajulikana kuwa ana nidhamu ya hall ya juu. Ni mtiifu, anafanya kazi zote za nyumbani na shuleni anaongoza. Wazazi hawa walijua fika kuwa Mungu amewajalia. Kwa imani ya dini, Safia alikuwa mcha Mungu kabisa.

➢  Ili kujitayarisha na mtihani wake wa mwisho, Safia aliomba rafiki yake aje kwao wadurusu pamoja. Wazazi wake bila shaka wakamkubalia. Kimwana aliyeaminika kuwa na tabia kama ya Safia akawa anakuja kudurusu. Wakimaliza alirejea kwao. Kuzuia usumbufu wa Lulua ndugu mdogo wa Safia, wazazi wakawaruhusu kujifungia ndani.

➢  Safia alianza kuwa mnyonge na kutapika. Mama mtu akaingia shaka. Alipomshirikisha mumewe, hakuafikiana  naye wakati walicheza aliwahi kujitoma chumbani akaingia shaka. Alipomshirikisha mumewe, nayc, V,ulua wakati walicheza aliwahi kujitoma chumban akawakuta Safia na shogake wamelala —na shogake ana ndevu Safia alikuwa mjamzito na katika shughuli za kutoa akafariki. Mimba ni ya shogake mwenye ndegu.

DHAMIRA

  • Mwandishi amedhamiria kuwakumbusha wazazi kuongeza umakini katika malezi ya watoto. Wasiwaamini watoto wao asihmia mia moja.

MAUDHUI Changamoto za Malezi

➢  Wazazi wanaweza kujitahidi kutoa malezi yanayofaa lakini maamuzi ya kuwa na

mwenendo bora ni juu ya mhusika mwenyewe. Mtoto wa Bi. Habiba Chechei aitwaye Mkadl alisemwa kuwa ana tabia chafu sana. Safia alionekana mwenye tabia nzuri. Na alipoamua kuwa mzuri alitekeleza majukumu yote —kusaidia kazi za nyumbani, kuheshimu watu na kutia bidii masomoni. Kwa upande mwingine aliamua kufanya mapenzi kabla ya wakati akijua kuwa sio vyema.

➢  Aidha anasema uongo kwa mama yake. Jitihada za Bi Hamida za kutaka ajue ukweli zikagonga mwamba. Safia akaarnua kutoa mimba ingawa alielewa ni kosa. Na alifariki. Akawaachia wazazi na jamii nzima mshangao na masikitiko

Unafiki na Uongo

➢  Safia alikuwa mnafiki na mwongo. Alijifanya kwamba ana tabia safi kama umande, kumbe alikuwa na tamaa ya ngono Wanakijiji wanamsema vibaya mtoto wa Hamida Chechei na kumfananisha na mbwa. Hawakumsengenya Safia kwa sababu mbele ya macho yao alikuwa na tabia nzuri. Mama anapomuuliza na kumdhihirishia kwamba anamshuku, anapandisha hasira. Baba Safia, Bw. Masudi, alimwamini binti yake mno, hata akakashifu fikra zake. Matokeo yake Safia anafikia hatua ya kudanganya kuwa yule anayesoma naye chumbani ni binti kumbe njemba yenye ndevu.

Tamaa za vijana

➢  Safia anajitahidi kwa kila jambo, masomo aliyamudu vyema. Anasifika kwa kazi za nyumbani kama vile kupika, kufua, kupiga pasi na kadhalika. Kanuni au sheria za dini alizizingatia bila wahaka (wasiwasi) wowote. Hata hivyo anawaka tamaa ya kufanya mapenzi. Anaamua kutumia ujanja kwa kutoa ombi ambalo halikuwa na shaka kwa wazazi wake. Na yeye akajichimbia kaburi mwenyewe

➢  “Kimwana” anaye anakuwa na tamaa. Alijifutika kwenye buibui na kujifanya kuwa yeye ni kimwana shoga yake Safia. Udanganyifu huo umeleta hali ya mtafaruku kwa wazazi wa Safia. Bi. Hamida anakosa furaha kabisa. Huenda njemba hii hatawahi kujulikana daima kwa kuwa muda wote ilijifutika buibui lililoficha use wake.

Umbea

➢  Bi. Hamida na wanawake wengine wa mtaani walikuwa wambea. Wamemkashifu na kumuumbua Mkadi, mtoto wa Habiba Chechei. Wanamwita kwamba yeye ni mbwa koko na uovu wake umezidi wa shetani. Bi. Hamida baada ya mtoto wake Safia kumwendea kinyume hataweza kusema lolote.

Bidii katika Kazi

➢  Kutia bidii katika shughuli yoyote zile huleta tija. Awali bidii masomo zilimpatia sifa nzuri Safia kwa sababu alikuwa wa kwanza hadi mwaka wa mwisho. Aidha bidii yake ya kazi za nyumbani, , staha yake na ucha Mungu ulitambuliwa na kila mtu.

Mikasa Maishani

➢  Bw. Masudi na Bi. Hamida walikuwa na maisha ya utulivu.Wanandoa hawa wawili walikuwa wanaelewana. Upendo na ushirikiano wao hujidhihirisha kwa vile wanavyozungumzia mambo mazito ya nafsi zao. Baada ya kufurahia mwenendo wa binti yao —furaha inakatika ghafla. Wanajikuta katika hali ya kupatwa na janga — janga la kifo cha ghafla cha mwanao na soni mbele ya macho yao.

Tabia na Mienendo ya Vijana

➢  Vijana mara nyingi huwa na mihemko ya kupapia mambo kabla ya wakati. Mkadi alikuwa na mwenendo usiofaa.Wanawake wambea akiwemo Bi. Hamida wakamsengenya.Safia naye katafuta njia ya kukidhi tamaa zake kwa njia mwafaka. Wazazi wake mwenyewe wakarahisisha mambo kwa kuwapa ruhusa ya kujifungia ndani. Sio rahisi kutambua mienendo ya vijana. Ni vyema kuviepuka vitendo viovu maana matokeo ya uovu hayafichiki. Bi. Hamida anaanza kutilia shaka unyonge wa Safia na kutapikatapika kwake. Shaka haikuwa uongo bali ukweli mtupu.

Hila na Ujanja

➢  Safia alitumia maarifa na ulaghai kuwahadaa wazazi wake. Alijua fika namna atakavyowateka akili bila hata kumtilia shaka. Ujanja wake na hila ukamwezesha kufanya mapenzi ndani ya nyumba ya wazazi wake. Dalili za mimba zilipoanza kudhihirika akasingizia homa ya malaria sugu. Alidanganya kwamba alienda hospitalini. Anapoona mama anam shuku, anatumia ujanja mwingine kuzibia hila zake- Anafanya hila za kuitoa mimba na hatimaye anaonja pepo mwenyewe.

Imani ya dini

➢  Dini ni dhana mwafaka ya kumwongoa mtu ili awe mnyofu. Hata hivyo dini inaweza kutumiwa visivyo. Safia alijifanya kwamba ni mshika dini mno —hadi wazazi wake hawakumshuku kwamba anaweza kuwaendea kinyume.

➢  Daima alijifunika ushungi hata akiwa humo ndani mwao.Anatumia mwamvuli wa dini kujificha na kufanya uovu mtupu.

MBINU

Methali

➢  Kuzaa mwana si pato, pato ni kumvyeleza (Uk 29)

➢  Lisemwapo lipo, kama halipo linakuja (Uk 30)

➢  Siri ya kata iulize mtungi (Uk 30)

➢  Kidole kimoja hakivunji chawa (uk 31)

Tashbihi

…bintiye aliye safi kama umande s

….hikamoo inayotoka nyuma ya buibui kama kata ya maji mtungini.

Mjadala wa nafsia/ uzungumzi nafsia

  • Bi. Hamida, baada ya kuona hali ya mwanae ya unyonge na kutapika.

Mdokezo

  • Kidugu kidogo cha Safia kilisimulia kisa shogaye kuwa na ndevu kwa kudokeza kidogo kidogo. Juzi… Juzi… Ivyo (Uk 34)

Taharuki

Baba Safia anapoelezwa juu ya kifo cha mwanae alishikwa na mshangao mkubwa. Hatujui vile alivyoathirika. Aidha hatujui vile mama yake Safia alivyochukulia jambo hilo.

WAHUSIKA

Safia

➢  Huyu ni binti wa Bw. Masudi na Bi. Hamida.

➢  Anasifika mno kwa tabia yake nzuri isiyokuwa na doa lolote

➢  Katika masomo yake alikuwa anaongoza darasa.

➢  Ana kipawa cha uzingativu wa kiwango chajuu.

➢  Ni msaidizi mkuu wa mama yake Bi. Hamida.

➢  Anamudu kazi zote za nyumbani.

➢  Anazifanya bila manung’uniko yoyote.

➢  Ni mwenye tamaa: anatamani kufanya mapenzi na akatumia hila kutimiza lengo lake.

Alikuwa amejivika ngozi ya kondoo nje, ndani mbwa mwitu.

➢  Ni mjanja: anatumia maarifa na hila za kila namna ili kupata fursa ya kufanya mapenzi.

➢  Ni mwenye hasira: Bi. Hamida anapomdadisi kuhusu hali yake ya kutapika, anapandisha hasira na kukimblha chumbani mwake.

➢  Ni mwongo: anadanganya kuwa ana malaria sugu-

Anadanganya kuwa Kimwana anakuja ili wajadiliane kumbe anayekuja ni mvulana mwenye ndevu na wanafanya rnapcnzi.

➢  Ni muuaji: anatoa mimba na kukidhulumu kiumbe kisicbO na hatia. Mambo hayakwenda sawa na yeye akafariki.

➢  Ana ubinafsi: anafikiria yeye tu bila kujua madhara ya kiurnbe kilichomo ndani tumboni mwake.

➢  Ni mchangarnfu: yeye ana tabia ya uchangamfu ndiornaana ora mama aliyabaini mabadiliko Baraka.

Umuhimu

  • Ujanja na hila zina mwisho wake. Mara nyingi huwa na mwisho mbaya.

Bi. Hamida.

➢  Mama yake Safia.

➢  Ameolewa na ana watoto wawili, Safia na Lulua.

➢  Anawapenda watoto wake na kuwapatia mahitaji yote.

➢  Safia anasoma Shule ya msingi na wanampa fursa nzuri ya kujitayarisha ili aingie sekondari.

➢  Ana upendo na msikivu kwa mumewe: huwa na masikilizano mema na mumewe Bw.

Masudi.

➢  Ni mchunguzi: aling’amua hali ya Safia mara tu alipoanza kubadilika na kumdadisi.

Ingawa Safia tabia zake ni nzuri sana, alitia shaka na kumweleza mumewe.

➢  Anamdadisi Lulua ili kutosheleza mashaka yake kwa Safia.

➢  Anajua ukweli kwamba kupata mtoto na kumlea ni mambo mawili tofauti.

➢  Mtimiza wajibu: anahakikisha kwamba Safia anapata mandhari mazuri yenye utulivu kwa ajili ya kudurusu.

➢  Anampa Safia mwelekeo kuwa akiwa ndani ya nyumba si lazima ajifunike gubigubi.

➢  Ni mbea: anamsengenya Mkadi, mtoto wa Habiba Chechei, kuwa ana tabia mbaya.

Anakiri kwamba anashiriki kwenye vikao vya kusengenyana akiwa na wanawake wenzake kila siku (Uk 30)

Umuhimu

Vijana wa kisasa wanatumia hila za kila aina kuwahadaa wazazi. Ni vyema wazazi wawe macho zaidi kufuatilia mienendo ya watoto.

1.5 SHIBE INATUMALIZA —Salma Omar Hamad

Muhtasari

Ni kisa kinachohusisha Mzee Mambo ambaye ni waziri kivuli wa wizara zote. Yeye mwenyewe anakiri kwamba hana kazi yoyote.

Hivyo yeye ameamua kutumia fursa hiyo ili kujishibisha, “…Mimi nipo kuongeza idadi ya walaji karamuni ” (Uk 37)

Jambo linalodhihirika wazi ni kwamba katika taifa Ia Mzee Mambo, hakuna uwajibikaji. Fedha za umma hutumiwa kiholela. Kinachotazamwa zaidi ni kuenda kazini na si kufanya kazi (Uk 37) Mzee Mambo hupakua mshahara yaani hujitwalia yeye mwenyewe. Yeye hapewi mshahara.

Baada ya kujipakulia mshahara, sasa kuna kusherehekea —kuna shangwe, hoihoi na nderemo.

Mzee Mambo anapokuwa na sherehe kuna wimbo unaopigwa daima. Wimbo wenyewe una fumbo ndani yake:

” …Mola ndiye atowae akampa mahuluki mali,

Humpa amtakae

huyo ndo humbariki. Na kila amnyimae kupata hatodiriki Mpewa

hapokonyeki, aliyepewa kapewa

Hata ukifanya chuki, bure unajisumbua  UK 37)

Wimbo huu unaonekana kukejeli wale wasio na vyeo. Wimbo huu unaonesha Mzee Mambo kashiba shibe kweli. Hii ni sherehe ya kusherehekea mtoto wake wa kwanza kuingia Shule ya chekechea

(nasari skuli).Yule wa mwisho ameota vijino viwili kutokana na

matukio hayo kuna sherehe kubwa.

Sherehe hiyo inarushwa moja meia kwenye televisheni ya Taifa. Aidha, inasambazwa kwenye mitandao Mingine yote ya mawasiliano.

Licha ya kupata uhondo wa kupakua mshahara, Mzee Mambo anaendelea kupewa tilt-sa ya kuhujumu mali ya taifa.

Katika sherehe ya Mzee Mambo, magari ya serikali yalipewa m: qukumu mengi; kuleta maji, mapambo, ikibidi kupeleka watoto

Wakati huu watu wanakula vyakula mbalimbali ingawa hakuna kupika. Kuna vyakula vya kubwakia, kutafuna n k. Aidha kuna vinywaji tele tele —vikali, vitamu n k. Vyakula vinavyoliwa hapo haxikutayarishwa. Basi kuna hatari kwamba vyakula hivyo sio

bora. Hata hivyo watu hawachunguzi.

Wakati wa mchana Sasa na Mbura walipata fursa ya kula vyakula.

hakula ambavyo wamevipata. Ingawaje wana haki ya kula vyakula hivyo vilikuwa vimenyakuliwa na watu wengine. Hivyo wanaviita yetu vyao!” yaani ni “vyetu lakini ni vyao ” (Uk 40)

Wakati muafaka walioungoja Sasa na Mbura unafika na wao wakajiunga kwenye foleni na kula kupita kiasi. Wakati huu wote mitambo inaendelea kurusha matangazo. Baada ya wao kushiba wanaanza ushindani usio wa msingi. Wanalinganishana aina mbalimbali za mchele —kati ya mchele wa Mbeya na Basmati.

Kutokana na shibe kubwa sasa anakumbuka shairi ambalo hnabainisha kwamba wale walalao wataamka baada ya kupata matatizo mbalimbali. Wakati huu wote matukio yanarushwa hewani.

Kuna Wimbo wa kejeli ambao waporaji wa mali ya umma. Hawajali hata wakilaumiwa. Yeye anaomba kuishi kwa amani na watu.

Wimbo huu unadhihirisha kuwa wanyakuzi wa mali ya umma hawajali. Wananyakua mabilioni kwa kutumia mbinu na hila za kila namna. Misingi na mipangilio yenye kunufaisha taifa hutupiliwa

Wanafungua maduka ya dawa zilizonyakuliwa kutoka kwenye bohari za serikali.

Wanapata huduma zote muhimu bure ilhali wenye kipato kidogo mno huzipata kwa malipo. Huduma ambazo wanyakuzi huzipata bure ni pamoja na; maji, umeme na matibabu.

Shibe waliyokuwa nayo Sasa na Mbura ziliwapa usingizi mzito. Wakagundua kwamba kula kunatumaliza (Uk 44)

ANWANI

  • Anwani ya hadithi hii ni “Shibe Inatumaliza”. Anwani hii imebeba maudhui yaliyomo barabara. Dhuluma, ufujaji wa mali za umma na ukandamizaji wa wanyonge ni matokeo ya shibe waliyonayo viongozi walioko madarakani. Mapuuza yote ya shida za wanyonge ni matokeo ya shibe ya watawala.

DHAMIRA

  • Mwandishi amedhamiria kubainisha namna viongozi serikali wanavyolewa madaraka na kufanya wanavyotaka. Mzee Mambo ni waziri asiye na wizara lakini anakwapUa mshahara mnono na anatumia mali za serikali kwa namna anavyotaka yeye.

MAUDHUI

Unyakuzi wa mali ya umma

➢  Kuna unyakuzi unaofanywa na viongozi mbalimbali. Kwa mfano Mzee Mambo ana cheo ambacho hakina wadhifa wowote serikalini. Hata hivyo yeye anajichukulia ujira au rnshahara wa kiwango cha juu mno. Katika kuendesha shughuli zake zote za kibinafsi anatumia mali za serikali —magari, madereva, mafuta n k.

➢  Fedha na mali za serikali zinatumiwa na wakubwa kwa shughuli duni zisizo na maana.

Mzee Mambo anafanya sherehe kubwa mno kwa sababu kifungua mimba ameingia

‘nasari skuli’ na kitinda mimba ameota meno. Vyakula vingi vyote vilivyoandaliwa ni mali ya umma.

Ubadhirifu

➢  Mali ya umma inatumiwa ovyo ovyo na hakuna anayejali. Magari ya serikali hubeba mapambo, maji na kadhalika.

➢  Huingia na kutoka kumshughulikia mtu mmoja. Vyakula vinavyoliwa na vinywaji ni vingi mno.

Mapuuza

➢  Makosa yote yanayotendwa na wakuu ya kuharibu mali yanapuuziwa —’sijali lawama’.

Hata watu waumie kwa kiasi gani wao hawajali. Viongozi wengine badala ya kuchukua hatua zifaazo dhidi ya wanyakuzi —wanangojea wakati muafaka ili nao wanyakue. Pindi wapatapo nafasi hutumia mwendo wa kasi kujinyakulia na kulimbikiza “NaSisi twende tusogee kule ” jungu lile linateremshwa.(Uk39)

➢  Vyombo vya habari vimemuangazia unyakuzi wa Mzee Mambo na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.

➢  Viongozi wananyakua mabilioni ya fedha lakini hawachukuliwi hatua yoyote. Haya ni mapuuza.

Ukandamizaji wa Wanyonge

Katika taifa la Mzee Mambo, wachochole hukandamizwa kwa njia nyingi.

  • Wao wana dhiki na ufukara.
  • Hulazimika kulipia huduma zote muhimu.
  • Wakubwa wanadai kuwa wanakula kwa niaba ya wanyonge.

WAHUSIKA

Mzee Mambo

➢  Ni waziri kivuli wa wizara zote. Aidha ni mkuu asiye na kazi maalum. Hivyo vyeo vyake viwili humtatiza yeye mwenyewe kwa kuwa hajui kazi yake hasa nini.

➢  Licha ya kutokuwa na majukumu yoyote, Mzee Mambo anapata mshahara mkubwa sana wa bure (hakuufanyia kazi)Hufurahia hali yake hiyo ya kupiga ubwete.

➢  Ni mbinafsi: hutumia vyombo vya umma kwa matumizi ya kibinafsi.

➢  Ni mbadhirifu: tukio dogo la kifungua mimbakuanza ‘nasari skuli’ linamfanya aandae sherehe kubwa mno. Kulikuwa na;

▪   Magari ya serikali hutumiwa ovyo ovyo —kubeba mapambo, kupeleka watoto kuogeshwa.

▪   Mitambo ya runinga za serikali inarusha na kuonyesha sherehe hii moja kwa moja (Huu ni ubadhirifu maana sherehe hii haina umuhimu wa kuonyeshwa na kituo cha Televisheni ya Taifa.

Umuhimu

➢  Mzee Mambo ni kielelezo Cha watu wanaopiga ubwete na kufuja mali ya umma kwa kulipwa mishahara.

➢  Ni kielelezo cha watu wa tabaka la juu ambao hawana uzalendo hata kidogo —kuifilisi serikali na hajali.

➢  Ni kielelezo cha viongozi wanaofuja mali ya vizazi vijavyo na kuwaacha bila chochote.

Sasa na Mbura

➢  Hawa ni mawaziri wa wizara moja. Ni Wizara ya mipango na mipangilio.

➢  Wanafanya kazi ngumu zaidi na wizara hii ndio muhimu zaidi

➢  Wanafanya kazi ngumu zaidi na wizara hii ndio muhimu zaidi kuliko zote.

➢  Wao hujituma ili kuhudumia taifa lao. Wanatengwa mbali na hawatambuliwi na taifa.

➢  Ni walafi: wanapopata fursa ya kupata mali, wanaitumia

➢  Wana mapuuza: ingawa wanafahamu uzembe uliopo na unyakuaji wa mali ya umma, hawachukui hatua mwafaka.

Umuhimu

  • Wametumiwa na mwandishi kudhihirisha jinsi wananchi wenyewe wanavyochangia katika kuzorotesha nchi —kwa kuachilia unyakuzi uendelee. Walioko madarakani wanakaa tayari kunyakua mara tu wapatapo fursa ya kufanya hivyo.

Mbinu

Jazanda

➢    Majina ya wahusika “Sasa na Mbura” yametumika kijazanda.Kusasambura ni kutoa nguo zote. Wahusika hawa wametumiwa kuonyesha vile ambavyo viongozi wanavyovua taifa Iao mali yote iliyokusanywa na vizazi vilivyopita. Aidha, wananyakua rasilimali hata za

vizazi vijavyo. Mali za serikali kama dawa zinatolewa katika bohari na wanyakuzi wanafungua maduka ya dawa.

Aina mbili za mchele

➢  Mchele wa basmati —unasimamia bidhaa duni zinazolundikwa katika nchi changa na mataifa mengine. Mawaziri wanaohusika hawaja chukua hatua yoyote.

➢  Mchele wa Mbeya: Vitu asilia vya nchini ni bora na vina manufaa zaidi.

Nyimbo

Mchele wa Mbeya: Vitu asilia vya nchini ni bora na vina manufaa zaidi.

Nyimbo

➢  Kuna nyimbo tatu zilizoangaziwa katika hadithi hii. Nyimbc hizi ni za dhihaka na kejeli.Wimbo wa kwanza unachezwa mara kwa mara MzeeMambo anapokuwa ana sherehe. Wimbo huu ni wa kufumba watu macho kuhusu chanzo cha mali ya Mzee Mambo inayotumika kiholela. Ujumbe wa nyimbo ni kwamba Mola ndiye anayempatia mja mali Yule anayemtaka. Na mtu akishapewa mali yake hawezi akanyang’anywa.

➢  Ubeti wa shairi unasikika baada ya Sasa na Mbura kula na kuwa katika usingizi wa mang’amumang’amu ” Ujumbe wa ubeti huu ni kwamba watu wakishalemewa na dhuluma za wakubwa itabidi waanze kudai haki zao “

➢  Wimbo wa tatu nao umejaa kejeli vilevile. Unabainisha wazi —’majuju’- watu wa hadhi ya Mzee Mambo kwamba hawajali lawama zinazotolewa na watu kuhusu vitendo vyao. Wanahiari watu wote wakae salama bila kulaumiana, na watu wakijitenga na kutojihusisha nao ni kuwadhulumtl

1.6 MAME BAKARI-Mohammed Khelef Ghassany

Muhtasari

Kitoto Cha Sara ambacho kilizaliwa kilifanya baba mtu aanze kumheshimu mwanae. Sara alipata mimba iliyotokana na kubakwa.

Baba yake akazidi kumpa bintiye heshima kama njia ya kumpa moyo na faraja iliyotokana na kisa hicho.

Kisa kinaanza kwa kuzingatia mashaka ya Sara msichana wa Shule ambaye alibakwa na lianaume fulani. Machozi yalimkurupuka yakamwagika njia mbilimbili. Alikuwa na majuto makuu ambayo yaliandamana na mishale iliyomchoma mwilini mwake. Kila alipokumbuka kisa hicho kilitonesha kidonda kwa upya ndani mwake.

Sara alibakwa Jumatano moja usiku alikuwa ametoka kwenye masomo ya ziada. Kisa hicho Cha kinyama kilinata akilini mwake, akawa anakumbuka kila kitu. Janadume lenye harufu kali ya kutuzi lilimvamia na kumbaka ghafla. Alijaribu kujipapatua lakini akazidiwa nguvu. Likambamiza ardhini na kumkandamiza. Sara alipoteza fahamu kwa nusu saa. Alipozindukana alifahamu wazi kuwa ameshapoteza uanawali wake.

Tukio hilo la kinyama, lilimsababishia Sara majonzi si haba.

Alijaribu kutatua shida yake. Akawaza na kuwazua. Hakumweleza baba yake maana alihofia hangesadiki tukio hilo na badala yake angemfukuza.

Sara alihofia vile ambavyo angeai bika, kutengwa najamii, ku fukuzwa

Shule na watu kusengenywa. Alifikiria jinsi ya kujiauni kwa aidha kujiua au kutoa mimba. Mambo hayo yote mawili hakuyaafiki.

Hawezi kujiua maana yeye hakuwa mkosaji, aliyekosa ni lile jitu. Yeye Sara hakudhulumu, bali ni mdhulumiwa. Wazo la kutoa mimba

Pia hakuliafiki. Kwa sadfa siku mbili kabla ya kubakwa alikuwa amesoma shairi la ‘Usiniuwe’ Ia

Abdullatif Abdalla, lihusulo utoaji

Wa mimba. Kitoto kichanga kilisema na mama yake tumboni. Sara

wazazi wa Sara mashaka yake kutokana na mapenzi yao wakaanza kumpa msaada. Baba mtu akaanza kumwita Sara mama. Wakagharamia matibabu yake yote. Wakampa faraja kuu wakati Sara alipopigwa na mshangao wa kuwakuta hospitalini ” Hapajaharibika jambo mama’ngu ” Mapenzi ya dhati kwa mtu aliyepatwa na janga kubwa kama hili ni tiba mjarabu.

Siri

➢  Mtu anapopatwa na shida nzito huhitaji kuiweka siri hadi wakati mwafaka. Sarina alitunza Siri ya Sara kwamba ni mja mzito. Aidha walipomweleza Beluwa naye aliahidi kuiweka Siri. Daktari Beluwa aliweka siri lakini akawa ametafuta dawa bora zaidi —ya kuwaeleza wazazi wao.

➢  Wazazi nao waliiweka siri hadi wakati mwafaka ulipotimia na hapakuwa na haja ya kuficha kitu chochote “hakuna haja ya siri hakuna haja ya hofu ” Hili lilileta faraja kubwa kwa Sara hatimaye akajifungua salama salimini.

Uhalifu

  • Yule nduli ambaye ndiye baba mtoto wa Sara, alitenda tendo la kinyama kwa msichana.

Msichana mnyonge na dhaifu, alijaribu kupigana nalo likamshinda nguvu. Hata hivyo uhalifu haulipi chochote. Alimdhulumu Sara na kutoroka akamwacha amezirai nusu uchi. Unyama huo unafikia mwisho wakati alipojaribu kubaka msichana mwingine.Aliadhibiwa vikali akautoa uhai wake. Wakati wa kipigo alitamani ahurumiwe lakini watu walimuua kabla polisi hawajafika.

  • Uhalifu una malipo yake. Watu walimwadhibu vikali hasa baada ya Sara kumwasa

“ulidhani uhalifu wako ungedumu milele

Maudhui mengine ni pamoja na

  • Kifo
  • Mabadiliko
  • Malezi
  • Elimu n k Mbinu Taswira.

➢  Kuna taswira ya chemchemi ya majonzi ya Sara ilipomwaga mito miwili. Inaonyesha

huzuni na majonzi makuu aliyokuwa nayo.

➢  Kitumbo chake kilichokwishaanza kufura. Hii ni inaonyesha mabadiliko ambayo yalijilazimishia kwa Sara baada ya kubakwa.

➢  Kuna taswira chafu ya janadume lililombamiza ardhini —kuonyesha ukatili wa tendo hilo.

➢  Kuna taswira hisi —ya mkandamizo na mdidimizo hadi akapoteza fahamu. Kuna aina nyinginezo nyingi za taswira katika hadithi hii.

Mjadala wa nafsi/ uzungumzi nafsia

➢  Baada ya janga la kubakwa kumfikia Sara alikuwa na mjadala mrefu wa nafsi. Sara alijizungumzia mwenywe;

– Ili kutafuta ufumbuzi alipohakiki chanzo cha yeye kufikiwa na janga hilo.

– Athari za tukio hilo n k

mbinu inayoonyesna dhana mbili tofouti zinazopingana

Dhana moja na kinyume chake. Kwa mfano: yeye ni mkosewa si mkosa. Ni mdeni si mdaiwa. Ni mdhulumiwa si dhalimu (Uk 50)

Mbinu rejeshi / kisegere nyuma

➢  Sara anarejelea Jumatano moja saa tatu na nusu akitoka stadi za ziada wakati

alipobakwa. Aidha, anakumbuka daima sura mbaya ya nduli aliyembaka na yale yote aliyopitia.

➢  Sara anakumbuka shairi la ‘Usiniuwe’ alilosoma shuleni na yeye akawa mtetezi sana darasani.

➢  Sara na Sarina wanakumbushana vile ambavyo waliapa kusaidiana wawili Pindi wapatapo shida ” Ahadi ya kale ni ile ile Sara”

Sadfa

➢  Ilikuwa sadfa kwa Sara kuwa mtetezi wa shairi la usiniuwe na siku mbili baadaye anabakwa. Na yeye akawa katika njia panda ya kutoa mimba au la “Sitakuua mwanangu kamwe”

➢  Wakati Sara alipobakwa ilisadifu kuwa uzazi wake ulikuwa sawa akashika mimba. Hii ni sadfa.

Balagha

➢  Haya ni maswali yasiyohitaji majibu. Ni kauli za kuleta uzindushi. Udhaifu na unyonge si ndio maana ya uanauke? Si kwa sababu ya umbile langu ndio mwili wangu ukatumiwa kukidhi utashi wao (Uk 48)

➢  Kwa nini hakutoa taarifa siku ile “Ati umebakwa? Nani akubake wewe?” (Uk 48)

➢  Sara anajiasa mwenyewe aache kulia kwa kujiuliza “Matone mangapi ya machozi amekwishajirovya?” (Uk 50)

Mawazo mk gizana. suluhisho mwafaka. k 50)

kila wazo likatangaza suluhisho mwafaka (uk 50)

mangapi ya machozi amekwtsna

Mawazo mkururo yakipangizana kila wazo likatang suluhisho mwafaka (Uk 50)

Tashbihi

  • “ ….Wengi mno ” na kumtenga kama mgonjwa wa ukoma (Uk

Jazanda

Mzigo kupata wachukuzi —tatizo likapata ufumbuzi.

Sitiari

Mwanamke ndiye shetani (Uk 48-50)

Taharuki

Kuna taharuki mwanzo wa kisa hiki. Msomaji haelewi nini Sara ana majonzi mpaka asome kisa zaidi “Je, lile ndul bakaji lilifumaniwa vipi na kulifululiza hadi karibu na

Sara “

WAHUSIKA Sara

Msichana wa Shule ambaye alibakwa akiwa ametoka kwenye stadi za jioni. Msichana mwaminifu ambaye amejitunza vema. Kitendo hicho kinamsononesha mno, hasa ilipoto kwamba jibakaji hilo lilimpachika mimba.

Sara anapata uchungu usioneneka na akawa anajisaka ni kwa nini machungu ya namna hiyo yalimfika. Je, ni kutokana na jinsi yake au unyonge. Alijaribu kubaini chanzo cha masaibu yake hayo yote. Baada cha kilio na uchungu mwingi anatoa

Hayazoleki . Anamweleza mwendani wake Sarina naye akauchukua mzigo ule kama wake. Hatimaye akafanikiwa kujiepusha na mzigo huo akajifungua salama.

Sifa take

  • Ni mwenye kupenda masomo: fikra kuwa angefukuzwa
  • Shule zilimtia moto na uchungu.
  • Ni msichana aliyejitunza: alilia sana kwa kuupoteza usafi wake wa kisichana.
  • Ni mwoga: aliogopa ukali wa baba yake baada ya kutendwa unyama na hakusema
  • Ana mapenzi ya dhati: yeye na Sarina wanapendana sana.
  • Ana busara: anaamua kuwa kujiua sio suluhisho mwafaka maana yeye siye aliyekosa.
  • Ana utu: hakutaka kuavya mimba kwa hivyo akakihifadhi kitoto.
  • Ni mwelewa wa jamii yake: alijua vile watu walivyo wanapenda kudodosa mambo ya wengine.

Umuhimu

Ametumiwa na mwandishi kudhihirisha uovu wa ubakaji na athari zake mbaya. Sara ni kielelezo cha vijana ambao hutumia busara zao katika kupambana na majanga ya maisha.

Sarina

  • Huyu ni mwendani wa Sara. Anapojulishwa mkasa wa Sara, anatia shaka kidogo halafu anampa kila aina za msaada.
  • Ni mwaminifu: alitimiza ahadi yao wawili ya kusaidiana.
  • Ni mwaminifu: alitimiza ahadi yao wawili ya kusal
  • Ni mcheshi: anamwonya Sara awe mwangalifu asibakwe tena.
  • Mkarimu: alikuwa tayari kumpeleka Sara hadi kwao shambani akajifungulie huko.
  • Mwenye hila na maarifa: anapanga mpango kuwa Sara avae jilbabu nyumbani na shuleni ili kuficha mimba.

Umuhimu Wake

Ni kielelezo cha marafiki wema ambao hukirimu wandani wao wakiwa katika shida.

Bakari

➢  Huyu ni baba yake Sara.

➢  Anaonyesha kuwa ni mtu mkali sana maana binti yake anashindwa na kumweleza tukio la kubakwa shuleni.

➢  Baadae anabadilika na kuwa mpole akampatia matunzo mtoto wake.

➢  Ni mcha Mungu: anafanya sherehe ya Maulidi baada ya mame Bakari kuzaliwa.

➢  Ana mlahaka mwema na majirani: anawakaribisha watu wote wakiwemo majirani.

➢  Ni mfariji: anamfariji mwanawe na kumpoza wakati alipoangua kilio katika chumba cha daktari.

➢  Mwenye mapenzi ya dhati: baada ya kugundua kuwa Sara ana himila alimheshimu na kumwita mama.

➢  Ni msiri: ingawaje walifahamishwa hali ya Sara mapema na mkewe, waliiweka siri na hawakuonyesha kama walifahamu chochote —hadi siku rasmi iliyopangwa.

Umuhimu

kutoa msaada kwa wanaodhulumiwa. Aidha, ni kielelezo

Cha wazazi ambao wako tayari kubadilisha msimamo mkali wa ulezi na kutoa msaada unapohitajika.

Janadume bakaji

➢  Nijitu lisilo na utu linalovizia wasichana usiku na kuwabaka.

➢  Ni katili: anambamiza Sara ardhini hadi akazimia na kumwacha hivyo.

➢  Lenye tamaa na uchu: baada ya kumbaka Sara aliendelea na tabia hiyo mbaya hadi akafumaniwa na kupigwa vibaya hadi akafa.

Umuhimu Wake

jadili

1.6 MASHARTI YA KISASA —Alifa Chokocho

Muhtasari

Kisa hiki kinahusu Kidawa mwanamke mrembo ambaye alipendwa na mvuvi na muuza samaki aitwaye Dadi. Dadi alimpenda sana

Kidawa na akataka amchumbie awe mkewe. Kidawa alimkataa

Dadi na kumkwepa kabisa. Hata hivyo mambo yalibadilika ambayo yalimshangaza sana Dadi. Kidawa alimwambia kwamba yu radhi kuolewa na Dadi kwa masharti ya ndoa ya kisasa. Dadi kwa shangwe alizonazo hakuzingatia undani wa Kidawa ” Ujue kwamba mimi ni mwanamke wa kisasa, na mwanamke wa kisasa hutafuta mwanamume wa kisasa mwenye mapenzi ya kisasa (Uk 58)

Dadi akamwoa Kidawa mwanamke wa kisasa. Baadhi ya mambo aliyotakiwa kuyatekeleza ni kusaidia kazi za nyumbani, kukuna nazi, kuosha vyombo, kufua na kupiga pasi. Pia amruhusu Kidawa afanye kazi ya umetroni kwa Shule ya wasichana usiku. Kidawa alifanya kazi hio kwa zamu. Aidha kidawa akawa na biashara ya kutembeza bidhaa za Uarabuni mitaani. Kidawa aliyafanya haya ili

“Kuunganisha ncha nyingi za mahltaji ya maisha ” (Uk 61) Baada ya miaka tisa ya ndoa, Dadi alianza kuingiwa na shaka. Akamshuku

Kidawa, akachukia kujipamba kwake, akachukia kwenda kufanya kazi usiku, akachukia alivyosimama na kuongea na wanaume wengine na vile vile akachukia uchuuzi wa bidhaa alizofanya.

Furaha ile ya kumwoa Kidawa hadi akaitwa Dadi kichekacheka kwa kumpata mke wa kisasa Kidawa ikamtoka. Chakula kikamshinda jioni moja. Masharti ya kuosha vyombo kwa zamu pia yakamshinda.

Dadi alimfuata Kidawa kazini ili kumfumania na mwalimu mkuu kama alivyoshuku. Dadi

akaenda nyumbani kwa mwalimu mkuu akaelezwa hakuweko. Ana kazi zilizomzidi shuleni. Dadi akawa na hakika ya kuwa mtego wake ungenasa. Mpango wake wa awali alivyopanga — akapanda paipu inayoelekea gorofani ili amwone mwalimu mkuu na Kidawa wake. Dadi

alikosea mwalimu alikuWa peke yake na rundo Ia karatasi akisahihisha. Kidawa alipojitoma

52

ndani alitaka kujiuzulu kazi kwa kuwa mumewe anamshuku.

Dadi alionekana juu ya paipu “Wewe nani? Unachungulia nini hapo juu? Wewe mwizi, nini? Au mpiga bodi… Nyinyi walinzi bwenini kuna mtu amepanda juu ya paipai anachungulia ndani, ” (Uk- 68).

Sauti iliwavutia Kidawa na mwalimu mkuu. Kidawa akakuta ni mumewe. Dadi aliangukia kokoto na damu ikamtoka kichwani.

Mwalimu mkuu akapiga simu kuita ambulensi.

ANWANI

Anwani ya hadithi hii ni “Masharti ya Kisasa”. Anwani hii inasawiri maudhui yaliyomo ndani yake. Mambo yote yanayomkuta Dadi yanatokana na yeye kutoelewa ni nini mke wake anachomaanisha anaposema “masharti ya kisasa”. Hatimaye anajaa wivu, wivu unaopelekea tatizo ambalo yumkini lingeweza kutwaa maisha yake.

DHAMIRA

Mwandishi amedhamiria kuonesha jamii kuwa wivu wa kupindukia ni hatari sana.

MAUDHUI

Migogoro ya wanandoa

➢  Kidawa alijua mabadiliko yaliyomo maishani. Ingawa wanaume wengi walimtaka yeye aliahiri yule atakayefuata masharti yake. Alimtaka Dadi atoe uamuzi. Dadi alitoa uamuzi bila kuelewa kwa undani. Kutokana na hayo kukaingia kutoaminiana. Ukale aliokuwa nao Dadi, na desturi za kitamaduni zikaleta mgongano. Laiti angalijua

➢  Kidawa alikuwa mwaminifu na kwake angetulia. Masharti ya kisasa aliyotoa Kidawa yalikuwa pia mageni kwa jamii. Dadi alihisi dunia inamchekelea. Yote haya ndiyo yaliyoleta

➢  Sio vyema Kudhamana Jambo hata hivyo, mtu anaposhuku kitu, ni vyema kutafuta njia nzuri na salama ya upelelezi. Njia aliyotumia Dadi ya kupanda paipu ilikuwa ya kubahatisha na kudhani kuwa hangeonekana. Kwa sadfa alionekanm

Ahadi maishani

➢  Kidawa alijua anataka maisha ya aina gani na akafanya uamuzi wake. Aliamua kuwa mume atakayemuoa afuate masharti ya kisasa. Dadi anapewa masharti na ayakubali. Alijitahidi sana kuyashikilia kwa miaka tisa. Hata akakubali kwamba wapate mtoto

mmoja kufuatilia usasa. Kwa Dadi hakuyaelewa yale masharti vyema baadae yanamletea karaha na maisha yake yakavia. Ni vyema kuchunguzajambo lolote vyema kabla ya kukubali masharti.

Elimu

➢  Elimu ni muhimu maishani. Kutokana na mwanga wa elimu mtu husika anapata maarifa na ujuzi wa kupanga maisha yake. Kidawa alimaliza kidato cha nne na akatumia ujuzi wake kuandaa maisha. Kuna wanaume wengi waliomtaka, akawakataa na kumfuata Dadi ambaye alimkubali “Wewe nimekupa mitihani mingi, na naona umefaulu ” (Uk 58)

➢  Kutokana na elimu duni ya Dadi, anaingiwa na shaka na kumshuku mkewe. Akaona kwamba japo hajasoma, amebaini kuwa Kidawa anamwendea kinyume. Ukweli kwamba Kidawa ni metroni na anaenda kazini usiku, na usiku, kukamzidishia Dadi fikra zake hizo Mume wake anafanya kazi ya kuuza samaki. Mja apatapo fursa ya kazi ni bora aifanye “

Kuunganisha ncha nyingi za mahitaji ” Msimamo wa Dadi kuhusu shughuli za Kidawa ni finyu na umepitwa na wakati. Kutokana na mapato ya kazi za Kidawa, anavaa vizuri na kujipamba atakavyo.

Urembo

➢  Mwanamke akivaa vizuri asichukuliwe kwamba ana macho ya nje. Kidawa alipenda kudumisha urembo wake. Dadi akamdhania anamvalia mwalimu mkuu. Kidawa alijimudu kwa ajili ya biashara ya uchuuzi —alitembeza bidhaa zake. Hayo yote Dadi aliyaelewa vibaya na vikamzidishia hofu isiyokuwa ya msingi.

Umbea na masengenyo

➢  Dadi alihofia minong’ono ya watu ambao walikuwa wanamsema kwa vile alisaidiana na mkewe. Jambo hilo likamnyima raha. Wanawake na wanaume walimsema kuwa alidhibitiwa na Kidawa. Jambo hilo linamwumiza mno. Walidai sio mwanamume tosha. Dadi anapozungumza na Zuhura anajishikilia ili asimpashe maneno makali akijua kuwa bibi huyo ni mmbea.

Itikadi na Utamaduni

kukuna nazi? Dadi anachukulia kuwa mwacha mila mtumwa, akasahau pia kuwa mwacha mila ni jasiri. Dadi hakuwa na huo ujasiri kutokana na msimamo wa jamii yake

Mapenzi ya dhati

➢  Dadi alimpenda mno Kidawa, hata alipopewa masharti ya kisasa Pindi wakioana aliyakubali bila kufikiria kwa makini maneno hayo baada ya miaka tisa anashindwa kushikilia masharti, akajjiumiza bure bilashi akitafuta ithibati.

➢  Kwa upande wa Kidawa naye alikuwa na mapenzi ya dhati. Wanapotembea njiani alimkemea Dadi —hakutaka aangalia wanawake wengine. Anapojipamba vyema alimwuliza mumewe ikiwa amependeza. Dadi alichukulia vibaya swali

WAHUSIKA

Dadi

  • Huyu ni mchuuza samaki. Alimpenda mwanamke mmojaKidawa kupita kiasi. Dadi alijaribu kumpata Kidawa kwa kila njia lakini hakuweza. Alikata tamaa kabisa. Kidawa alibadilisha mtazamo wake. Dadi akapewa masharti ya kisasa katika ndoa yao. Hayo masharti yanamuumiza rohoni na kumsononesha.
  • Hajiamini: kutojiamini kwake kunatokana na elimu duni aliyokuwa nayo.
  • Ana bidii maishani: anachuuza samaki kwa bidii hadi wamalizike.
  • Hana msimamo: anayumbishwa na maneno ya watu hadi akakosa raba kabisa.

mwalimu mkuu na kupanda paipu ili kuhakikisha. alilipanga kwa siku nyingi.

Umuhimu

Si vizuri kuzingatia tuhuma kabla ya kuhakikisha. Sio rahisi kuleta mabadiliko katika jamii.

Kidawa

Mwanamke mrembo ambaye alitaka kuolewa na wanaume wengi. Aliwakataa na kuwachuja hadi akamchagua Dadi.

Yeye alisoma hadi kidato cha nne. Alitaka mwanandoa ambaye angezingatia masharti ya kisasa ya ndoa.

Ni mzingatifu: anajua alitaka nini maishani na akazingatia matakwa yake —ya ndoa ya kisasa.

Ni jasiri: mwacha mila ni jasiri. Hakuyumbishwa na umbeya wanajamii kama Dadi.

Umuhimu

Kidawani kielelezo cha mwanamkewakisasa ambayehatakl kushikilia mila za kizamani. Ni vyema mtu atoe msimamo wake maishani ili ujulikane bayana.

Mnunuziwa samaki. Mwenye manenoya karaha. Anakashifu samaki wa Dadi na kudhani kuwa wameoza.

Ni mmbeya: anampiga Dadi vijembe kuhusu anavyoindesha ndoa yake.

Umuhimu

Ni kiwakilishi cha wanawake wambeya wanaojiingiza kwenye mambo ya watu.

Mwahmu Mkuu

Mwenye utu: anapiga simu mara moja kuita ambulensi baada Dadi kuanguka na kuumia kichwani.

Mbinu

Taharuki

Baada ya kupelekwa hospitali, Je alipona au aliaga dunia, ukizingatia kuwa aliumia vibaya kichwani. Je, Kidawa alikichukuliaje kitendo hicho cha mumewe kupanda juu ya paipu na kuchungulia ndani?.

Taswira oni

Kuna taswira ya Kidawa akiwa amevalia viatu vipya na kanzu tayari kwenda kazini usiku. Zipo taswira nyingine nyingi.

Aidha kuna taswira ya kile chakula cha jioni cha ndizi na samaki ambacho Dadi hakukigusa kwa wivu.

Sadfa

➢  Dadi alienda kuona iwapo mwalimu alikuwa kwake jioni.Alipomkosa akajihakikishia kwamba alienda kukutana naKidawa.

➢  Aidha ilikuwa sadfa kuwa taa ya nje ilikuwa haiwaki naDadi akapata mandhari mazuri ya kujificha akipanda ile paipu.

Kuchanganya ndimi

Kuna maneno ya Kiingereza yaliyotumika kama “Stop your gaze!” my dress my choice celeb, socialite n k.

Mdokezo

  • Kidawa alijaribu kumhakikishia mumewe uaminifu wake na kumkumbusha ahadi zao, alipogeuka na kuona chakula hakikuguswa alikatisha usemi wake (Uk 66)
  • Dadi alipokuwa akienda shuleni kumwangalia mwalimu mkuu, alijiapiza kuwa leo ni leo na hakumaliza msemo huo.
  • Wakati mwalimu mkuu alipokuwa akimwasa Kidawa kuhusu kuacha kazi, mdokezo umetumika “Mtu ana kazi nanga zinapaa, sikwambii “(Uk 68)

Takriri

Neno kisasa limerudiwarudiwa kusisitiza kiini cha hadithii hii “Mwanamke wa kisasa hutafuta mwanaume wa kisasa, mwenye mapenzi ya kisasa (Uk 58)

Misemo

  • Nyota ya jaha (Uk 57)
  • Pweleo la tamasha (Uk 56)
  • Kugeuka maji kuzima moto (Uk 57)

Koja

Mapenzi ni mateso, ni utumwa ni ukandamizaji, ni udunishaji, ni ushabiki ni ugonjwa usio dawa

(Uk 56)

Tashbihi

…kama anga lolote Ia dunia (Uk 57)

Tanakuzi

Matumiziyamaneno yanayopingana. Waliosoma wasiosoma wenye uwezo na wasio nao (Uk 57)

NDOTO YA MASHAKA – Ali Abdullah Ali

Muhtasari

Hadithi hii inaanza kwa kusimulia uzuri wa ua la waridi na umaarufu wake. Linapendeza na kunukia vizuri. Ni ua lenye haiba. Waridi linasimamia msichana ambaye Mashaka alimpenda mno. Ua lake la waridi lilikwanyuka kwanyu likachukuliwa na upepo. Hivyo ndio

Waridi wake alivyotoweka siku moja.

Mashaka alikuwa na makuzi ya mashaka kama jina lake. Alikuwa na mama mlezi Biti Kidebe, maana wazazi wake wote walifariki

Pindi alipozaliwa. Mashaka amekua katika ukata hadi kifo cha Biti

Kidete. Alikuwa wa kufanya vibarua vya kila aina. Yalikuwa makuzi ya tikiti maji au tango, ya kuponea umande (Uk 57)

Mashaka aliozwa Waridi kwa kufungishwa ndoa ya mkeka. Hii ndoa, hufungwa kwa kushtukiza, pale wazazi wa binti wanapomfuma binti yao yuko kwa mwanaume. Waridi na Mashaka walikuwa wakipiga gumzo humo chumbani mwa Mashaka. Mlango ukapigwa teke na

Mzee Rubeya, akaingia akifuatana na shehe. Wakafungishwa ndoa.

Mzee Rubeya kwa kuwa ni mkwasi, aliona aibu binti yake kuozwa na mtu hohehahe. Yeye na familia yake wakakimbilia Yemeni.

Hali ya Mashaka ya ukata ilizidi. Waliishi chumba kimoja na watu tisa! Yeye mkewe na watoto saba. Mandhari hayo yalikuwa duni.

Walikaa karibu na choo ambacho hufurika mvua inaponyesha.

Mabinti walibanana kwenye kitanda kidogo na wavulana walilowea kwa jirani. Mwenyewe

Mashaka ni mlinzi wa ZWS —Zuia Wizi

Security.

Maisha yao yalijaa dhiki ” Dhiki ilikuwa ndiyo nguo na harufu yetu. (uk 76)Siku moja alipofika kwake hakumkuta Waridi wala watoto.

Alipofikiri vizuri akaona wimbo aliopenda kumwimbia Waridi ulikuwa na ujumbe wa kumwaga

” .Nashundwa kuvumilia mie bora nirudi kwetu ” (uk 77) Baada ya hapo Mashaka alibakia akiota

61

61

ndoto tu. Hali ya ya arnbao ulimsababishia adha kadhaa;

  • Kama sio ukata mke wakc angernheshirnu
  • Asingemtoroka
  • Angekuwa na fcdha kumfrahi%ha yeye na watoto
  • Watoto wangcmpenda yeye Pia
  • Na yeye angejipcnda.

Mashaka aliwaza na kuwazua akatathmini na kutafuta idadi ya

Mashaka Tandale alikoishi na kwingine duniani ‘Kuna Tandale ngapi Kenya, kuna Tandale ngapi

Uganda kuna akina Mashaka wangapi Afrika nzima (Uk 78)

Anashangaa kwa nini jamii za kimataifa hazitaki kuukemea mfumo huu. Mashaka alijituliza na kujiasa kuwa awe na subira. Hata hivyo hakusaidika.

Katika hali ya kimawazo na kuota baada ya karne moja, Waridi ua lake lilimrudia, akaufurahia uzuri wake na harufu. Kabla ya hapo kulikuwa na maandamano makubwa ya wanyonge. Wasakatonge waliandamana ‘Tunataka tufe! Bora tufe! Walibeba mabango na kupiga kelele zilizofika kila mahali. Kelele zao zilipenya kama radi kwa watu wa matabaka ya juu.

Maandamano yalibadilisha kila kitu. Utabaka ukaisha. Maisha polepole yakawa bora. Mashaka akawa na Waridi mkewe. Alifajirika mno. Kwa ghafla kumbe hiyo ilikuwa ndoto, Mashaka akaamka akajikuta yu pale pale katika umaskini wake.

ANWANI

Anwani ya hadithi hii ni Ndoto ya Mashaka.

maana mhusika mkuu anaitwa Mashaka. Naye alipatwa na

82

alifariki Mashaka alipomaliza chumba cha nane. Mashaka anaozwa binti wa tajiri Mzee Rubeya alipogundua kuwa wanapendana. Ndoa yenyewe ya mashaka. Shehe na Mzee

Rubeya waliwafuata Waridi na Mashaka walipokuwa wanapiga gumzo —chumbani na kuwafungisha ndoa. Ndoa hii ilileta aibu kwa familia ya Rubeya na wakahamia Yemeni alikotoka. Mashaka alipata watoto saba. Ufukara ukazidi kipimo. Waliishi katika chumba kimoja kile

kibovu. Shida ziliposhamiri mkewe alitoroka na watoto wake. Mara nyingi aliota ndoto ya kuwa

Waridi ua lake limerudi, lakini ndoto ikiisha anajikuta yuko pweke kwa mashaka yake. Hivo kisa hiki kinasadifu kuitwa ‘Ndoto ya Mashaka ‘

MAUDHUI Mkosi maishani

  • Mashaka alikuwa na mkosi tangu alipozaliwa. Wazazi wote walifariki akiwa mchanga.

Alipata mlezi ambaye alikuwa fukara. Mashaka aliishi kwa kufanya vibarua ili kumsaidia

  • Biti Kidebe mlezi wake. Alipomaliza tu chumba cha nane —mama mlezi akafariki.

Mashaka anaoa binti mrembo lakini kutokana na ufukara anamkimbia yeye na watoto saba. Licha ya kupigana, mkosi wa ufakara ulimwandama.

Tabaka la chini

Mwandishi anaangazia suala la utabaka. Anadhlhirisha kuwa kuna watu wengi maskini. Ingawaje wanajaribu kupigana nao bado hawajawahi kujinasua. Mwandishi anatoa tathmini pana ya chanzo cha umaskini. Anaonyesha kuwa katika mtaa wake wamo maskini wengi. Na si humo tu, kuna sehemu nyingi nyinginezo. Watu wa tabaka la chini wanakaa sehemu zisizo na mpangalio maalum wa ujenzi.

63

anawaa senemu zisizo na mpan

63 o

Chumba cha Mashaka kwa mfano kimepakana na chm cha jirani. Maji ya kuogea yanapita kanbu na chumba cha chao. Watu wanaoishi katika mandhari haya ni wenc

Mvua ikinyesha kundi Zima hili huwa mashakani Vlongozi hutangaza kuwa watu wa bondeni wahame lakini hawapewi mahala mbadala.

Watuwa tabaka la chini au wasakatonge hujitahidi kupigana na kujitoa humo lakini hawajafaulu. Pengine huandamana na kubeba mabango lakini hawafaulu na juhudi huishi patup x

Tabaka la chini hubaguliwa, Mzee Rubeya anahamia na kurudi Yemeni maana hakuweza kustahimili aibu ya binti yake kuolewa na mchochole.

Ukombozi

Wasakatonge wanaona kuwa, hali zao zinakatisha tamaa.

Wanapanga maandamano ili kujikomboa. Waliandamana huku wanapiga kelele “Tunataka tufe! Bora tufe! Walifikia kauli hii kwa sababu walichoka kusubiri. Waandamanaji wanazidisha kelele

zao, hadi wakandamizaji waliotia nta maskioni wanalazimika kusikiliza na mambo kubadilika. Utabaka ulififia na hali mpya ikaanza. Hata hivyo kwa kuwa haya yote yalikuwa kwenye ndoto ya Mashaka ni dhahiri kwamba ukombozi halisi haujakita mizizi na kufaidisha wananchi.

Ujenzi wa jamii mpya

Mwandishi anaangazia kwamba kuna umuhimu wa kupunguza pengo la kitabaka ili kuleta usawa. Mazingira mapya yataleta matumaini kwa kina Mashaka. Hata hivyo hiyo itatokea tu wakati sauti za wachochole zitakapoweza kusikika.

Mjenzi mpya utafikiwa ikiwa wachochole watapiga moyo konde na wasilegeze juhudi zao “Katika maandamano yale walikuwa wamefura na kufuriana. Walizidi kuumuka kama vile hamira ya hasira iliyowaenea miilini (Uk 81)

Mjenzi mpya utafikiwa ikiwa Wachochole watapiga moyo konde na wasilegeze juhudi zao

“Katika maandamano yale walikuwa wamefura na kufuriana

Walizidi kuumuka kama vile hamira ya hasira iliyowaenea miilini (Uk 81)

64

Muundo

➢  Hadithi hii ina muundo usio sahili. Kuna sehemu zilizogawanywa kwa vinyota. Kila sehemu inabeba maelezo tofauti. Sehemu ya kwanza inaeleza juu ya Waridi binadamu na waridi ua wakati huo huo. Katika msuko wa maelezo hayo ameelezea sifa za waridi

ua na Waridi binadamu yaani mkcwe. Sehemu hiyo pia inakuwa kama muhtasari wa kisa kizima. Tuligandamana tukawa kitu kimoja mpaka pale dhoruba ilipotutenganisha (Uk

71).

Baada ya kitangulizi hicho msimulizi anaelezea kisa kilichokuwa kimetokea kabla ya sehemu hiyo ya kwanza, iliyotengwa kwa kinyota. Hapa anaeleza usuli wake na mikasa yote iliyomsibu. Sehemu inayofuatia kwa mtiririko mmoja, inaelezea juu ya ndoa yake ya mkeka.

Baada ya nyota (Uk 74) anaelezea maisha ya ndoa yao. Hadi sehemu inayoonyesha maisha ya ndoa. Usimulizi wa mkewe alivyomkimbia na mashaka yaliyompata unafuata.

Sehemu ya mwisho ina kitangulizi au anwani isemayo; ‘Siku nyingi tena ‘ Sehemu hiyo inaonyesha ndoto na mawazo yake aliyokuwa nayo. Akajumuisha mashaka ya wachochole na mikakati yao ya kujikomboa ambayo mwandishi anafikiria kwamba huenda ikachukua miaka na mikaka.

WAHUSIKA Mashaka

Kama lilivyo jina lake alikuwa na maisha ya mashaka. Ni yatima aliyelelewa na Biti Kidebe mwenye roho nzuri lakini mnyonge. Mama mlezi wake alimsomesha hadi darasa la nane. Alipata mkasa wa kumpoteza mlezi wake baada tu ya kumaliza Shule ya msingi.

Alikuwa na bidii: alifanya vibarua vya kila namna kumkimu

Biti Kidebe.

➢  Ni maskini: alizaliwakatikaufukaranajuhudazakezakujitoa hazikufua dafu.

➢  Ana mapenzi ya dhati: aliwapenda watoto na mke wake, wanapomkimbia anasononeka.

➢  Mwota ndoto: mawazo yake na subira kuhusu kujinasua kutoka makucha ya ufukara yanamfanya daima aote ndoto.

➢  Anapata faraja sana katika ndoto lakini anapata hangaiko la akili, akiamka na kukuta ni ndoto tu.

➢  Ana nyota ya jaha: alibahatika kupendana na binti mkwasi na wakafungishwa ndoa. Hata hivyo familia hiyo haikuwa saidia wakaendelea kusalia katika ulitima.

➢  Mwenye majuto: anajutia hali yake ya ufukara na kutamani angeweza kupata suluhisho

Ia kudumu.

➢  Mwenye tamaa: anatamani kupata fedha ili wanawe wafurahi wampende na yeye ajipende.

Umuhimu

Kwa kupitia kwa mhusika huyu, msimulizi anadhihirisha kuwa ni vigumu kumaliza duru ya uftkara. Mzazi akiwa fukara ni rahisi mtoto awe fukara vivyo hivyo.

Anadhihirisha kuwa mapenzi hayachagui, yanaweza kuota Ukata una misingi mipana inayotokana na mfrmo wa kimataifa. Waridi

  • Ni binti wa rnzee mkwasi Rubeya.
  • Ingawa anatoka katika familia ya kitajiri, anampenda yatima maskini Mashaka. Aliolewa na Mashaka wakapata

66

Alitvtpcnda Maghaka na baba yao alipoona hivi ndoa.

  • Mstahmiilivu: alimvumilia Mashaka kwa muda rnrefu watoto saba, Mtantauka: alikata tamaa ya kuwa na maisha ya ahueni hiVY@) akaamua kutMdi kwao, Mtot: antetomka kwa mumcwe na watoto wote saba bila kuwasiliana naye tena.
  • Mbinafsi: anampoka mumewe watoto wote bila kujifikiria kwamba mumcwc angckuwa mpwcke kupita kiasi.
  • Msiri: hakudokezea mtu yeyote kule alikokimbilia.

Umuhimu

Ametumiwa na mwandishi kudhihirisha kuwa mapenzi ni kama majani, huota mahali popote pale.

Mzee Rubeya

  • Huyu ni mkwasi mwenye asili ya Yemeni. Alioa mwanamke wa Kimanyema na wakapata watoto. Ni baba yake Waridi.
  • Anamfungisha bintiye ndoa ya mkeka. Hii inatokea baada ya kufahamu kwamba bintiye anamtembelea Mashaka chumbani mwake.
  • Alimchukua Shehe Mwinyimvua Mansuri kakake Waridi naIdi rafiki wa Mansuri. Kitendo cha bintiye kuolewa na mkata kilileta mtafaruku katika familia. Kulichukuliwa kuwa ni fedheha kuu; Mzee Rubeya akaamua kurudi Yemeni.
  • Anathamini usafi wa wasichana katika ndoa ndio maana aliwafungisha ndoa kwa mkikimkiki.

Umuhimu

Ni kielelezo cha watu wa tabaka Ia juu ambao hawataki kuchangamana na tabaka la chini.

6B 82

Mbinu

Kuna matumizi ya nyimbo

  • Wimbo wa kwanza ni wimbo wa kuhimiza watu wathamani na kula aina duni ya ndizi ambayo inaweza kufaa ikipata mpishi bora. Wimbo wa pili, umenakiliwa kutoka Redio Tanzania. Huu unatumiwa kuonyesha kuwa Waridi alipomwimbia mumewe Mashaka alikuwa anampa kidokezo kuwa anaondoka kurejea kwa wazazi wake.

Methali

  • Baada ya dhiki faraja (Uk 70)
  • Apewaye ndiye aongezwaye (Uk 75)
  • Kitanda usichokilalia huwajui kunguni wake (Uk 75)
  • Jungu kuu halikosi ukoko (Uk 72)
  • Siri ya mtungi iulize kata (Uk 75)
  • Ngoja ngoja huumiza matumbo (Uk 79)
  • Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha (Uk 79)
  • Kila chenye mwanzo kina mwisho (Uk 81)
  • Pangu pakavu (Uk 78)
  • Liwalo liwe (Uk 81)
  • lwe iwavyo (Uk 71 )

Tanakali za sauti

➢  Kokoko iikoo (Uk 82

➢  Kwa kwaa (Kwan. Uk 82)

➢  Puu ngwaaa (Uk 73)

➢  Pruuu. Pwaa (Uk 75)

Si ya sasa, si ya baadae (Uk 81)

Kinaya

Mzee Rubeya tajiri mtajika wa ukoo wa Mwinyi anamuo bintiye kwa kijana hohehahe.

Takriri

Miguuhiyo mie nitaingianayo kaburini! Eemiguu migt gani hii (Uk 72)

Jazanda

Kibuyu hakifichi mbegu (Uk 72). Mashaka anarejelea vi ambavyo siri hazifichiki.

Taswira

  • Kuna taswira oni —wanyonge wakiwa wamebeba maband yaliyoandikwa kwa wino uliokoleza (Uk 81)
  • Kifafa cha uzazi kilimpiga dafrau akaanguka chini —Pich ya mama Mashaka ya kufa ghafla.

Tashhisi

  • Rangi ya urujuani ilichungulia katika nyufa (Uk 82)
  • Kitanda changu cha mayowe kikapiga ukelele (Uk 82)

Tashbihi

  • zimepotea bilashi kama moshi (Uk 81)
  • kufuriana kama unga uliomwagiwa hamira (Uk 81). .Rubaa ya watu wane ikajitoma chumbani kama askari wa Fanya Fujo Uone (Uk 73)

Sitiari

Dhiki ndiyo nguo na haruiil yetu.

Balagha

Hadi lini lakini hadi lini subira hiyo (Uk 79) Matshaka akifikiria ukata wake unavyochukua muda mreli*. Je kuna

Tandale ngapi Tanzania (Mashaka akiwaza juu ya idadi ya maskini ) Kuna akina Mashaka wangapi (Uk, 78). Balagha zingine ziko Uk wa 72, 75, 76, 78, 80

Ndoto

Baada ya Waridi kumkimbia Mashaka aliota ndoto, kwarnba wanyonge waliandamana wakadai haki zao kwa nguvu, Walisubiri lakini hawakufaulu. Wakaanza tena harakati zao. Wakati huu wakawa wana hasira zaidi na wakazidisha kelele. Pia wakabeba mabango yenye ujumbe mkali zaidi.

Mabadiliko yakaanza, na wanyonge wakapata maisha bora.

Mashaka naye alikuwa miongoni mwao walioishi katika mazingira mazuri… Nilijiona nimezaliwa upya katika kizazi kipya (Uk 82)

70

70

1.8 KIDEGE – Robert Oduri

hupenda kwenda kubalizi upepo na kuburudishwa kwa mandhar yoke. Joy na Achesa wanaonekana wakivinjari mahaba yao katlk, bustani hii. Wanagaragazana katika viunga vya bustani hii, ilimrad tu wanajifurahisha. Mose naye anapendelea kutembelea bustan hiyo.

Katika bustani hii, kuna kidimbwi cha maji. Ndani yake visamaki vidogo vyenye rangi anuwai za kuvutia. Aidha, kidege ambacho kimezoea kuonekana hapo. Mose amezoea kubeb sima mfukoni mwake. Akifika katika kidimbwi hicho huvirushi visamaki sima. Wakati mwingine Mose huenda bustanini hapo n rafiki yake Shirandula. Shirandula yeye ni mzaliwa wa shamb

Shrandula anadai kuwa visamaki hivyo ni vidogo kuliko vil vilivyoko kijijini. Visamaki hivyo havifai kuvuliwa na kuliwa.

Siku moja Shirandula alimtegea Mose kitendawili. Kitendawi hicho kilitaka kujua ni yupi bora kati ya mjenga choo na mjeng kasri. Mose aliomba siku kadhaa ili atafakari jibu la kitendawi hicho.

Katika kutafuta majibu ya kitendawili hicho, Mose anaona mideg mikubwa yenye midomo kama panga. Midege hiyo ilikuu imekizunguka kile kidimbwi chenye visamaki vya kuvutia. Mideg ile ilikuwa ikijadiliana namna ya kujengajamii. Ndipo ikakubaliar kuwa kujenga jamii ni kula vitu vyote ambavyo yanadhani vidogo. Midege ile ikaanza kurarua vile visamaki. Mingine ilikuu ikinyanganyana.

Mose anashindwa kuifukuza ile midege. Mara kinakuja kile kide

mikubwa. Videge vile vinashuka kwa kasi ya ajabu na kuparu macho ya midege mikubwa. Vinatia sumu fulani katika macho ye ile midege. Mara midege inaanza kutapatapa na hatimaye kukimbia na kutoweka.

Mose alikuwa anashuhudia mtifuano ule wa videge vidogo dhidi ya tmdege mikubwa. Anafurahia kuiona midege mkubwa inafukuzwa na videge vidogo. Hatimaye kitendawili kinateguliwa kwa Mose kugundua kuwa mwenye choo ndiye hunya na mwenye kasri hawezi.

ANWANI

➢  Anwani ya hadithi hii ni Kidege. Anwani hii inasawiri maudhui yaliyomo ndani ya hadithi hii. Kidege ni ndege mdogo ambaye anaashiria wanyonge wa tabaka Ia chini. Wanyonge hawa wanakandamizwa kwa kudhulumiwa na midege mikubwa ambayo inaashiria tabaka la mabwana wenye nguvu. Hadithi hii inaeleza namna videge vilivyoungana kwa wingi wao na kuifurusha midege ambayo imevamia bustani na kuanza kuvirarua visamaki vilivyokuwa kwenye kidimbwi.

DHAMIRA

  • Mwandishi wa hadithi hii amedhamiria kubainisha kuwa umoja na mshikamano ndiyo nguzo imara ya mnyonge. Kama wanyonge wakishikamana, kwa umoja wao wanaweza kuondosha wavamizi wote wanaowadhulumu rasilimali na haki zao.

Maudhui

Dhuluma na Unyonyaji

Mwandishi anatumia midege mikubwa kubaini%ha suala I;

dhuluma na unyonyaji.

Videge vikubwa vinavamia bustani na kuanza kula vis vilivyokuwa katika kidimbwi.

Katika kuvizia na kunyakuwa visarnaki, midege hii inaharibl mazingira ya bustani hiyo. Midege inajadiliana namna ya kujenga jamii. Inakubalian;

kuwa kujenga jamii ni kula kila kitu kinachoonekana kidogo kwao (Uk 92).

Hii inaashiria namna wanyonge wanavyopokonywa; rasilimali na tabaka lenye mabavu katika jamii.

Inaashiria kuwa mijadala inayofanywa na viongozi waliok( madarakani inalenga wao kujinufaisha na rasilimali za taifa Kwao, ujenzi wajamii ni kubeba rasilimali zote za taifa kw manufaa yao.

Matabaka

Hadithi hii inabainisha kuwapo kwa matabaka mawil katika jamii ambayo yako katika mapambano.

Kuna tabaka la midege mikubwa. Hii ina nguvu midomo yao ni kama mapanga.

Midege mikubwa inavamia na kutwaa vi vilivyokuwa katika kidimbwi cha bustani ya Ilala. Tabaka hili la midege mikubwa linaashiria tabaka

timu, vilivyokuwa katika kidimbwi clot bustani ya llala. Tabaka hib la midege mikubwa linaashiria tabaka la -matajiri; watu wenye nguvu za k iuchumi katika Watu hawa hutumia nguvu zao kuwadhulumu wanyonge rasilimali na haki zao. Kwa upande mwingine kuna tabaka la videge vidogo ambalo linaashiria tabaka la wanyonge katika jamii. Tabaka hili la videge vidogo linaungana na kupambana dhidi yauvamizi wa midege. Hatimaye videge vinashinda na kuifukuza midege mikubwa

Umoja na Mshikamano

  • Hadithi hii inabainisha kuwa nguvu ya mnyonge ni umoja na mshikamano.
  • Videge vidogo vinaungana kwa wingi wao na kuamua kupambana na midege mikubwa.
  • Videge vinashikamana kuparua macho ya midege mikubwa na kuyatia sumu.
  • Videge vidogo vinashinda mapambano hayo na kufanikiwa kuifukuza midege mikubwa.
  • Hii inaashiria kuwa wanyonge wakiungana na kushikamana wanawcza kuwaondoa wanyonyaji wa rasilimali za jamii.
  • Penye umoja no mshikamano pana ushindi.

Muundo

  • Hadithi hii imetumia muundo wa moja kwa moja.
  • Kimeanza kisa cha Mose kutembelea bustani no kuwaona Joy na Achesa wakivinjari mahaba yao bustanini.
  • Kisha kikafuata kisa cha urafiki wa Mose, kidege na visamaki. na mapama ambayo yamefanikiwa kuiondosha midege hiyo vamizi.

Mtindo

  • Hadithi hii imetumia mtindo wa masimulizi (monolojia)kwa kiasi kikubwa
  • Kwa kiasi kidogo, mtindo wa mazungumzo umetumika.
  • Nafsi zote tatu zimetumika ingawa nafsi ya tatu imetawala kwa kiwango kikubwa

Taharuki

  • Kuna taharuki ya kujua wapi mapenzi ya Achesa na Joy yameishia. Je, baada ya bustani kuvamiwa na midege waliendelea kuvinjari eneo hilo?
  • Kuna taharuki ya kujua kama Mose alifanikiwa kuonana na Shirandula na kumpatia jibu lake. Kama alimpa jibu, kuna taharuki ya kujua kama jibu hilo lilikuwa sahihi.

Tamathali za Semi

➢  Tanakali Sauti, kwa mfano: .shwii shwaa shwii shwaa shwlll. “(Uk83)…pu!, chwiii ” (Uk 84)

➢  Misemo na nahau, kwa mfano: . binadamu nao na hamsini zao. ” (Uk87)

LB

➢  Taswira, kwa mfano:

Kidege/videge —huashiria watu wanyonge katika jatr, ii huashiria watu wenye nguvu za kiuchuthii

Midege —Huashiria watu wenye nguvu za kiuchumio/

kiutawala wanaowanyonga wanyonge.

Visamaki —huashiria rasilimali zinazoporwa na watu nguvu na mamlaka ya kiutawala.

WAHUSIKA Mose

➢  Ni kijana ambaye bado ni mwanafunzi

➢  Amezaliwa mjini

➢  Ni rafiki yake Shirandula ambaye amezaliwa kijijini

➢  Anapenda kutembelea bustani ya Ilala

➢  Anapenda kutazama visamaki kwenye kidimbwi cha bustani hiyo

➢  Anapenda kuvirushia visamaki hivyo sima kila anapotembelea bustani hiyo

➢  Anaambiwa na Shirakunda kuwa kijijini kuna visami vikubwa kuliko hivyo vya mjini

➢  Anatamani siku moja naye afike kijijini na kujionea

➢  Anashuhudia midege inavyovamia, kuharibu bustani na kuia visamaki vilivyokuwa kwenye kidimbwi

➢  Anashuhudia namna videge vidogo vinavyoung kupambana na midege mikubwa na hatimaye videge vibgo vinashinda

76

Mose anajitolea kulisha visamaki kwenye kidimbwi ambavyo vimekuja kutwaliwa na mabwana wenye nguvu

Shirandula

➢  Ni rafiki yake Mose

➢  Yeye amezaliwa kijijini

➢  Ndiye alimwambia Mose kuwa kjijini kuna samaki wakubwa kuliko wa mjini

➢  Alitega kitendawili kilichotaka kujua yupi bora kati ya mjenga choo na mjenga kasri

Umuhimu wake

  • Anarejelea vijana wenye weledi wa kueleza jambo kwa mafumbo.
  • Ameonesha kuwa na uelewajuu ya kuwapo rasilimali nyingi kijijini kuliko mjini.

Achesa na Joy

  • Hawa ni wapenzi.
  • Wanafurahia mapenzi yao katika bustani.
  • Wanapogaragazana bustanini, Achesa ananyewa na kidege puani.
  • Hata hivyo wao wanatazamana na kucheka kisha wanaendelea kufaidi huba lao.

UmuhimU

Ni kielelezo cha watu ambao wanaendelea na maisha bila kutilia manani juu ya kile kinachoendelea katika jamii.

TAMRINI

  1. “Hanyee mwenye kasri, hunyaa mwenye Choo ‘ a. Bainisha muktadha wa dondoo hili

(Alama 4)

  1. b. Fafanua sifa za wahusika wa dondoo hili

(Alama 16)

  1. Fafanua maudhui manne yanayojitokeza katika hadithi hii. (Alama 20)

Muhtasari Wa Tumbo Lisiloshiba Na Hadithi Nyingine (pdf Download)

Subscribe
Notify of

22 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments

Great job. it makes learning more easier

It’s awesome just simple& easy to learn

Thanks for providing content for free.

Thank you very much for your provisions.

nice stuff

lt’s a very nice guide;really understable!

thanks for providing this itatusaidia kama wanafunzi

Nice content. However, my daughter is unable to download the content. How can we go about this?

hadithi nyengine aziko toka ya tisa hadi kumi na tatu

thank you for this. it has been of really great help. God bless you.

in deed a nice job

five star to yot guys

Good work,continue

in deed a nice job

this a story missing eg mkubwa that is the last one

Keep It Up ,it Is So Awesome.

perfect for a student to score an A

I love this ❤️..it has make learning to be easier

Thank you very much NABISWA

It trully makes learning easier.

the notes are brief and somehow incomplete statements are used

Great thanks

wpDiscuz
22
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x
Exit mobile version